Njia Yako ya Emmausi

YOUR ROAD TO AMMAUS

Dini nyingi za uongo na waalimu wa uongo siku za leo wanamwonyesha Yesu mwingine tofauti kabisa na yule bibilia imeandika kuhusu. Ni Yesu wa bibilia pekee anayeweza kukuleta kwa wokovu na kukupatanisha na Mungu. "Msiposadiki kuwa mimi ndiye mtakufa katika dhambi zenu" (Yohana sura ya 8ms24), basi hebu tuangalie Yesu wa bibilia ninani, na kasha utaweza kutambua wa uongo.

Ilikufa hivi ni vyema kutazama nyuma katika kitabu cha mwanzo, kama vile Yesu alivyofanya alipotembea na kuzungumza na wanafunzi wake baada ya ufufuo wake Luka sura ya 24 ms 25-27. Hii itakuonyesha Yesu pekee ambaye amekubalika na Mungu na kwanini tunaamini Yesu alistahili kuzaliwa na mwana mwali na kufufuka kimwili.

Mwanzo sura ya 3 inatuambia kufukuzwa kwa Adam na hawa kutoka bustani ya Edeni kwa sababu walitenda dhambi moja tu, kula tunda la mti wa kujua mema na mabaya. Shetani akionyeshwa kama nyoka, akamjaribu Hawa kwa kumwambia kutoamini neno la Mungu, na aamini kuwa yeye na Adamu wakuwa kama Mungu mwenyewe. (Mwanzo sura 3 ms 1-6).

Huu ni mfano wa kile ambacho shetani mwenyewe alikuwa amefanya, mbinguni kujaribu kuwa kama Mungu mwenyewe. Baadaye Mungu alipokuja kumtembelea Adamu na Hawa, iliashiliki nao, walikimbia wakachificha. Kupitia maswali aliowauliza Mungu aliwapatia Adamu na Hawa kama nafasi tatu za kukiri na kutubu dhambi yao lakini badala ya kufanya hivyo, walijaribu kulaumu mtu yeyote isipokuwa wao wenyewe.

Hukumu basi, ikawa itolewe juu yao. Mungu akawafukuza kutoka bustani mwa Edeni kwa sababu walikuwa wamekula tunda la mti ambao aliwaonya wasile. Katika mstari wa 22 Mungu akawaza "iwapo sita waadhibu watoke katika bustani hii watakula la mti wa uzima na wataishi milele"

Mungu hakuogopa mwanadamu kuishi milele, kwa kuwa aliwaumba katika kusudi hili, na kuwa na ushirika naye, lakini aliwafukuza kutoka bustani iliwasile tunda la mti wa uzima ili wasije wakaishi katika dhambi yao milele, bila ukombozi.

Hii ikiwa sababu, Mungu ana hitimisha mpango wake kwa Adamu na Hawa (mstari wa 15), kuwa kupitia mmoja atakaye zaliwa na mwanamke (uadui kati ya mbegu yako na yake), atakuja atakaye mponda nyoka kichwa chake-kwa njia nyingine, kumponda kabisa chini ya mguu wake. Ushawahi sikia mtu akiambiwa "Anafanana na babake?" kumaanisha anaonyesa tabia zingine za babake.

Iwapo babako alikuwa na udhaifu, wacha tuseme upande wa wanawake, iwapo hutakuwa mwangalifu sana, utaonyesha udhaifu huo maishani mwako pia. Hii inaonekana wazi katika hadithi za Abraham na Sarah, na mwanao Isaka na mkewe Rebeka, hali zote mbili zinakalibia kufanana. Katika Mwanzo 20 Abraham anadanganya kuhusu Sara kuwa dadake kwa sababu anaogopa wanaweza kumuuwa

na wamchukue Sara kwa sababu ni mrembo, na katika sura ya 26 Isaka mwanaye, anafanya jambo hilo kwa Rebeka.

Udhaifu wa Abraham na hofu zinaonekana kwa Isaka pia. Kwa sababu sasa dhambi imeingia katika maisha ya Adamu, iwapo babake Yesu angekuwa baba wa dunia hii, mwanadamu, udhaifu wa dhambi ungelidhiwa. Basi, ikiwa adhabu ya dhambi ni kufukuzwa kutoka uweponi mwa Mungu, mwokozi anayestahili pekee ni yule asiyekuwa na asili ya dhambi ndani yake.

Baba wa mkombozi wetu lazima angekuwa Mungu, au angelidhi dhambi basi akose kukubakika na Mungu hata kujikomboa mwenyewe. Ukiwa tazama viongozi wa dini yeyote ya uongo (walioazisha kundi hilo)utapata kuwa wote walikuwa na baba wadunia , kwa hivyo ni vigumu mno wokovu kuja kupitia wao au kundi lao.

Kama vile yeyote aliye na asili ya dhambi hakubaliki na Mungu, chochote wanachofanya hakiwezi kuwafanya kukubalika, kwa sababu wataendelea kuwa na asili yao ya dhambi, kwa hivyo kama vile nyuma katika Mwanzo sura ya 3 imedhibitishwa kuwa hatuwezi kujipatanisha na Mungu, basi tunahitaji mtu ambaye hana dhambi kutufanya kwa niaba yetu.

Hii inajitokeza wazi katika mwanzo sura ya 4 mstari 1-5, ni hadithi ya Kaini na Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, Kaini alikuwa mkulima. Kaini akapaleka sadaka yake kwa Mungu, sehemu kutoka bustani yake au shamba lake, ambayo aliifurahia.

Hata hivyo nduguye Habili, akamtolea Mungu mwanakondoo, kwa ufupi alitwaa kondoo wa kiume na wakike katika uwaja mmoja na akaacha asili ifanye ipendavyo. Kaini sadaka yake, kwa msingi kazi ya mikono yake mwenyewe haikukubalika na Mungu, ingawa alipendezwa na sadaka ya Habili. Inapandeza kuona Yohana Mtakatifu alionyesha Yesu kuwa "Mwanakondoo wa Mungu".Alikuwa kweli mwanakondoo ambaye Mungu kupitia yeye atamwokoa mwanadamu?

Kilichofanyika kwa Abraham katika mwanzo sura ya 22 mstari 1-14 ni muhimu sana katika mafundisho yetu. Katika hadithi hii Mungu ana mwambia Abraham atoe sadaka ya kile ambacho ni cha dhamani kwake, mwanawe wa pekee ambaye Mungu alikuwa amemwahidi yeye mwenyewe na Sara. Abraham akamtii Mungu mpaka kiwango cha kutoa sadaka.

Akamweka Isaka juu ya kuni kama sadaka ya kutekateza na alikuwa ameelekea kumwangamiza wakati malaika wa Bwana alipasa sauti. Kabla Abraham hajamweka Isaka juu ya kuni, amtoe sadaka, Isaka akauliza swali la kawaida lakini swali muhimu. "yuko wapi mwanakondoo wa kutoa sadaka?" (msitari wa 7). Nina shaka iwapo Abraham alitambua umuhimu wa jibu alilotoa.

"Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka." Unapoona utaona Mungu alitoa sadaka sawasawa na ile Abraham alikuwa karibu kutoa. Abraham alikuwa amejitayarisha kutoa sadaka ya dhamani anachoweza kutoa, mwanawe pekee wa ahadi, Isaka, na baadaye Mungu akawa amtoe mwanawe wa pakee, Yesu, kwa ukombozi wa mwanadamu.

Malaika wa Bwana akamwita Abraham kabla hajamwua Isaka. Kwa hivyo wakati wote tunampotolea Mungu chochote tunachoona nicha dhamani kwetu, Naye anaturundishia, pamoja na baraka tele, katika haya yote na njia zingine Mungu akaendelea kufunua mpango wake wa kumwokoa mwanadamu.

Katika Misri mahali ambapo Mungu alikuwa ameahidi kuweka idadi kubwa ya watu huru kutoka kwa utumwa na kutoka njia ya uchungu ambayo walionyeshwa, Mungu akamchagua mtu ambaye kupitia yeye atawatoa watu hawa kutoka inchi hiyo kufika mahali ambapo watakuwa huru, mtu aliyechaguliwa alikuwa ni Musa.

Wakati Musa alitoa idadi hii kubwa ya watu kutoka utumwani Misri. Mungu akamwita, yeye peke yake wakutane naye mlimani, mahali Musa alikaa kwa muda wa siku themanini mchana na usiku. Hapo Mungu akamwonyesha vitu vingi vya mbinguni, pamoja na kiti chake cha rehema mahali ambapo damu ya sadaka ya dhambi itamwagwa kwa utakaso.

Kama vile alivyoagizwa, Musa akatengeneza hiyo hapa duniani. Mahali ambapo vitu hivi viliwekwa paliitwa hema ya kukutanika. Kisha Mungu akaamuru watu kwa kabila zao na akawapa nafasi katika hema hiyo ya kukutanika, mahali uwepo wa Mungu ulikuwa. Katika mkona wa kuume mbele ya mlango wa hema ya kukutania aliliweka kabila la Yuda. Hii ikaonyesha iwapo yeyote, sana sana mwokozi aliye ahidiwa, angetoka uweponi mwa Mungu, na wangetoka kupitia kabila la Yuda (Hesabu sura ya 2).

Baada ya kufanya haya yote Musa akapeana amri ya sadaka ya wanyama ya kutakasa jamii yote kutioka kwa dhambi. Wanyama aina nyingi wahitajika, kulingana na sababu ya sadaka, lakini wakati mwingi ilikuwa wambuzi wawili wakiume na mwanakondoo asiyekuwa na mawaa, au hawatakubalika na Mungu kama sadaka (Mambo ya walawi sura ya 16 mstari wa 10 Kutoka 12ms5 na hesabu sura ya 12 ms 46 tazama hizi) Kulikuwa na wakati mwingi wa siku za mwandamo wa mwezi na sherehe zilizo hitaji sadaka, tugeuke na tutazame nyakati mbili kuu za sadaka, ya kwanza ni sherehe ya Pasaka, wakati Malaika wa Bwana aliwaua wazaliwa wakwanza wa wana na wanyama wa Wamisri, lakini kwa sababu ya kutii kwao, maagizo yake, hakuna mtu wa Wahebrania aliyajeruhiwa.

Katika wakati huu waaliambiwa watoe sadaka ya mwanakondoo asiyekuwa na mawaa, wachome na waweke sehemu ya damu yake ambayo ingeondolewa kabla ya kupika, kwenye miimo na vizingiti. Wakati malaika wa kifo atayembelea mahali hapo, yeyote aliye ndani ya nyumba zilio na damu kwenye miimo ya nyumba hatapata madhara kabisa.

Kifo hata hivyo kitawapata watu wote waliokuwa hawana ishara hii kwenye kiingilio cha nyumba zao. Waliofanya hivyo waliagizwa wale mwanakondoo haraka, na wasibakishe chochote mpaka siku inayofuata. Hii ilikuwa inaonyesha kuwa kazi ya Masihi katika siku zake za mwisho itatimizwa haraka (Kutoka sura ya 12 ms 21-46).

Kabla ya sherehe na kutakaswa sadaka zinatangulia, ili lazimika idhibitishwe nini kuhani na kuhani mkuu watavaa na kufanya. Moja ya vitu viliokuwa vivaliwe nivazi refu nyeupe, niyo simamia utakatifu, imefungwa kiunoni kwa kamba ndefu. Chini ya vazi hili, kuzunguka upindo wake kulikuwa na kengele.

Iwapo sadaka iliyotolewa na kuhani au kuhani mkuu ilikuwa kwa njia yeyote na mawaa, huyo kuhani au kuhani mkuu ataangamizwa kwa kifo. Watu walioko inje watajua kuna kitu kasoro, wakiwa hawawezi kusikia kengele zikilia tena, kuhani anapozunguka katika hema ya kukutania, basi watashika kamba ambayo ilikuwa ndefu hata kufika nje ya hema ya kukutania na wamvute kuhani nje akiwa amekufa.

Iwapo kuhani au kuhani mkuu atatoka nje akiwa salama watajua kuwa sadaka imekubalika na Mungu na dhambi zap zimeondolewa. Siku ya utakaso – ambayo ilikuwa ni kutakasa jamii yote, kuwafanya safi na kuwafanya wakubalike mbele za Mungu, ilihitaji sadaka ya mbuzi wawili.

Moja atolewe katika sehemu ya kwanza ya hema ya kukutania, moja atupwe aende jangwani baada ya kuhani aliyechaguliwa ameweka mikono yake juu yake, kuonyesha amehamisha dhambi zao kwa mbuzi ambaye atatupwa aende jangwani, hivyo kutoa dhambi katika mkutano (Mambo ya Walawi sura ya 16 ms 1-10).

Sadaka ya ng’ombe mume na kondoo mume na mwanakondoo – kwa ajili ya dhambi za jamii itatolewa ndani ya hema ya kukutania, na damu yake kunyunyuziwa katika sehemu ya madhabahu na kwa kiti cha rehema. Mungu aliahindi kuwa iwapo haya ya ngefanywa inavyostahili, anapo tazama chini ataona damu ya sadaka isiyokuwa na mawaa juu ya kiti cha rehema na hii itaondoa dhambi za jamii.

Hii hata hivyo ilirundiwa kila mwaka kama vile watu waliendelea kutenda dhambi. Iliamliwa kuwa sadaka hizi zingetolewa "katikati ya jioni mbili". Kulingana na sehemu ya siku ya Wayahudi, iliyoanza saa kumi na mbili asubuhi (6am) katikati ya jioni mbili inamaanisha juu ya saa ya tisa (Kutoka sura ya 12) siyo saa tisa asubuhi au saa tisa jioni lakini saa ya tisa, ambayo itakuwa saa tisa jioni kulingana na mpangilio wetu wa mchana, Mambo haya yote yalikuwa na uzito wa muda mfupi, lakini ya likuwa ni ishara ya mambo yatakayokuja ya milele.

Basi ni wakati wakuangalia ni kiasi gani cha mambo yaliyokuwa yana hitajika ambayo Yesu alitimiza ili kutukomboa. Ya kwanza, imewekwa wazi kwamba mtoto aliyezaliwa na Mariamu alikuwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Mungu mwenyewe. Ilikuwa ni mbegu ya Hawa (mwanamke) aliyemtunza na kumzaa. Mathayo sura ya 1 ms 16 inatupatia ukoo wa Yesu kupitia Yusufu, mtu ambaye amechaguliwa awe baba wa Yesu hapa duniani, na Luka 3 ms 13 – 28 inapeana ukoo wa Yesu katika upande wa Mariamu.

Zote zina kubaliana kuwa ukoo wa Yesu unarudi mpaka kwa kabila la Yuda. Tukisha sema haya yote, lazima twende mbele tuangalie Yesu alifanyika kama Kuhani Mkuu wetu, sadaka ya mwanakondoo na mbuzi aliyetoweka jangwani ilituepukane na ghadhabu ya Mungu. Kabla ya kufanyika Kuhani Mkuu wa jamii, Kuhani Mkuu aliagizwa aoge na ajifunge kitambaa. Kupitia kusoma kile Yesu alichofanya na wanafunzi wake katika usiku wa chakula chake cha mwisho na wanafunzi wake tunaona wazi Yesu alioga akajifunga kitambaa(Yohana 13 ms 1 – 15).

Baadaye Yesu akapelekwa mbele ya Pilato na mashitaka ya uongo, na akapelekwa nje ya mji asulibiwe. Kama mbuzi aliyetoweka alikua atolewe nje ya kambi, Yesu alipelekwa nje ya kuta za mji (Yohana sura ya 19 msitari wa 17). Na akavikwa taji ya miimba kichwani mwake na alikuwa bila shaka anakiri dhambi za Israeli na dhambi za jamii yote, na pia ulimwengu wote (Mathayo sura ya 27 ms 27 na Yahana sura ya 19 msitari 22 – 24).

Kama ilivyokuwa ni chukizo kuuacha mwili juu ya msalaba siku ya Sabato, na kuhakikisha kuwa amekufa sasa kabisa, wakavunja miguu ya wahalifu wawili waliosulibiwa pamoja na Yesu na walipofika kwa Yesu wakapata tayari amekufa, basi kulikuwa hakuna haja ya kuvunja miguu yake (Yohana 19 ms 31).

Muda mfupi kufika saa tisa mchana, saa ya tisa ya Wayahudi, katikati ya jioni mbili, Yesu akapasa sauti kutoka msalabani "Yamekwisha" (Yohana sura yw 19 ms 30). Alisema hivyo kwa kuwa kwa wakati huu alikuwa ametimiza kila kitu duniani kwa kikamilifu kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wote, milele yote.

Ili kuhakikisha kuwa amekufa askari wa Kirumi akamdunga Yesu mkuki ubavuni mwake kukatoka damu na maji, Yesu alikuwa na anaonyesha Maisha yake yeye mwenyewe, na damu yake kama toleo mbele ya Mungu ilikwamba tusamehewe (Yohana sura ya 19 ms 31 – 37). Jumapili iliyofuata, ilikuwa siku aliyofufuka kutoka kwa wafu.

Sio kwa wokovu wetu, alikuwa tayari ametimiza hayo kwa ajili yetu, lakini kama vile jamii ya Israeli walijua sadaka ya dhambi zao imekubalika wakati Kuhani Mkuu alitoka nje akiwa hai kutoka uweponi mwa Mungu, basi Yesu akafufuka siku hiyo ilikutuonyesha kuwa Mungu amepokea sadaka yake na dhambi zetu sasa zimeondolewa iwapo tutaamini tu na kumwamini.

Kwa njia hii tunafanywa washilika wa jamii. Sasa jamii ni kubwa kuliko jamii ya Waisraeli, ni jamii ya waumini wa takaoishi milele. Sadaka hii ilikuwa ya dhamana kwa Mungu, msamaha na ukombozi umehifadhiwa sio wa mwaka mmoja, lakini ni wa milele yote. Tumshukuru Mungu.

back to main articles page