Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokolewa

Whoever believes and is baptized will be saved

Ubatizo kwa mkristo ambaye hana ufahamu kuwa yeye ni mgonjwa, sio jaguo, lakini ni amri. Ikiwa mtu kwa moyo wake wote amempa Yesu maisha yake na baada ya masaa machache ana kufa, ni na amini kuwa ikiwa walikuwa na moyo wa kupanga, na kupokea ubatizo wa maji, basi wokovu wao umehakikishwa.

Hebu sasa tuangalie ni kwa nini mtu ana hitaji kupokea ubatizo. Ya kwanza ni kufuata mfano wa Yesu, ambaye yeye mwenyewe alibatizwa katika mto Yordani (angalia Mathayo 3ms13-mwisho), kwa hivyo, tunastahili tufuate mfano wake nasi wenyewe tubatizwe. Ya pili, Mtume Paulo katika Warumi 6 ms3-11, anapendekeza huku kufa kiroho kwa dhambi ya maisha yetu binafsi tunapo kuwa tunatupukuzwa majini, na kuinuka kuanza maisha mapya katika kristo tunapotoka ndani ya maji.

Wakati mmoja mwalimu alikuwa akitoa somo kwa darasa lake, na katika mwisho wa somo lake, vijana wawili wakamjia wakamwuliza, "jina lako la pili ni Marko?" Mwalimu akatulia kwa sababu ni watu wachache waliokuwa wanajua jina lake la pili, "Ndio" akasema, watoto wale wakaondoka, wakarudi kesho yake kwa masomo, walipouliza swali lingine. "Je, ulizaliwa 13 machi 1936?"

Mwalimu akashikwa na mshangao ni vipi wanapata kweli hizi kumhusu, akasema "ndio". Tena akafikiria hilo kidogo, mpaka wakati watoto walirudi na swali linguine siku ya pili. "Je, uliugua na kufa tarehe mbili ya mwezi wa Agosti 1959?" Watoto waliuliza hivyo. Mwalimu alikuwa hawezi kukumbuka kugua huko basi akawauliza walikuwa wanapata wapi hizo habari.

Ambapo walijibu walikuwa wanawasiliana na kuzimu kupitia ujawi na uganga.Mwalimu kisha akakumbuka hiyo ndio siku aliyo batizwa kwa kuzamishwa kwa maji mengi, kutangaza Yesu kama Bwana na mwokozi wake. Kile ambacho watoto walifunua ni kwamba mapepo wachafu na roho wachafu wanamwona mtu ambaye amebatizwa kwa kuzamishwa kwa maji mengi kama "aliyekufa" kwao. Hata kama wanaweza kudhulumu na kuzuia mtu huyo, wanajua kuwa nafsi yake iko salama milele kutoka kwao, kutoka kitendo cha ubatizo.

Matendo 19ms17, inaonyesha kuwa katika siku za mitume, waumini walibatizwa na Roho Mtakatifu mara tu walipo batizwa kwa maji. Ingawaje kwa wengi hili haliko hivyo leo, inawezekana kuwa ingawa watu wengi wangetaka kupokea ubatizo wa maji, imekuwa ni jambo la kawaida kuwaombea ubatizo wa Roho Mtakatifu Siku tofauti, tukio la baadaye; kama inawezekana kufanya yote pamoja kwa tukio moja, ni vyema sana.

Maneno ya Mtume Paulo "Msilewe kwa mvinyo lakini mjazwe kwa Roho Mtakatifu" katika Waefeso 5ms18 liko katika kitendo cha kuendelea -kwa njia nyingine jazweni kila wakati na Roho Mtakatifu wa Mungu. Luka sura ya 11 ms 9-13 inasema kitu ambacho ni wakristo wachache wanakifamu kabisa leo. "Baba wenu wa mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?"

Basi kwa wazi tutaomba kujazwa Roho Mtakatifu siku baada ya siku, na kiasi tunachotaka na kuomba kitakuwa ndicho hicho utakachopokea kwa imani. Uliza kidogo na hicho ndicho utakachopokea, omba kwa imani kiwango cha juu nawe utapewa.

Inavyowezekana, kuzamishwa kabisa (mili yetu mizima kuingia chini ya maji kwa wakati mmoja) ndio mfano wa bibilia na mfano wa Yesu. Ninapendekeza iwe ndiyo kawaida ya leo pia. Iwapo mtu mgonjwa hawezi akaingia ndani ya maji mtu huyo pia anaweza kumwagiwa maji juu yake, kwa kuwa Mungu anaangalia zaidi moyo wa ndani wa mtu kuliko mtazamo wa nje.

Basi enendeni mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza wanaume na wanawake kila mahali, kwa jina la Baba, la Mwana na Roho Mtakatifu, hata ukamilifu wa dahari." (Mathayo 28ms19-mwisho)

back to main articles page