Silaha Zote Za Mungu Kwa Ufupi (Kutoka Waefeso sura ya 6)

The Full Armour of God (based on Ephesians chapter 6)

Kweli viunoni

The belt of Truth

Kweli ni muhimu sana kwa mkristo ambaye atakuwa mshindi na kumshinda muovu. Kuna msemo ambao unasema hakuna madhara kunena uongo mweupe, lakini hakuna kitu kama hicho. Kila tunaponena uongo tunakuwa sehemu moja na ibilisi, ambaye ni baba wa uongo, Kuwa wenye kweli kila wakati inamaanisha hatuwezi tukalegea tena, lakini kila wakati kutangaza ukuu wa Yesu, ikiwezekana pasipo kusababisha kosa.

Isipokuwa mtu ameamini katika ukuu wa Yesu wa injili, basi yote tunayemwamini ni kama kiongozi mwingine wa dini na mwazilishi, ambao wote hawana uwezo wa kulipia adhabu ya dhambi zao wenyewe, ambazo ni chache kuliko dhambi za mwanadamu kwa umilele.

Watu wengi wanafundishwa upotevu wa injili ya kweli, wengine wakipokea wokovu kwa njia ya matendo mema, wengine wanaambiwa ni kuwa na imani pamoja na matendo mema iliwaweze kupokea wokovu. Katika Waefeso sura ya kwanza, Mtume Paulo anasema waziwazi kuhusu injili anayo hubiri. "Umeokolewa kwa neema, kwa imani ndani ya Yesu mwana wa Mungu, sio kwa matendo mtu asije akajivuna."

Tunaona kweli ya hili na Abraham katika kitabu cha Mwanzo (Agano la kale) na kitabu cha Waebrania (Agano Jipya) kuwa Abraham aliamini neno la Mungu na hii ndiyo Mungu alihesabu kumhesabia haki. Ingawaje katika mambo mengine imani pasipo matendo sio imani kabisa, matendo yanayo zungumziwa ni, matunda ya kutoka katika uhusiano wetu na Yesu Kristo na bayana ya kazi ya Mungu katika maisha yetu, haya hesabiki kwa kupokea wokovu wetu, hiyo ni Imani hupewa kila mtu kama kipawa kutoka kwa Mungu. Kipawa ni kitu ambacho hatukupata kwa kizi yetu wala kustahili, tumepewa kwa neema sio kwa kujitoa kwetu kama sivyo hakingekuwa kipawa kabisa, lakini ni malipo ambayo yamefanyiwa kazi. Neno imani awali katika tafsiri halisi lilimaanisha zaidi ya kuikili, ilionyesha kitu ambacho umejenga maisha yako ndani yake. Imani ni kumwamini Mungu na kufanya anachokuambia ufanye.kupitia imani ndani ya Yesu kristo pekee.

Hili inaweza kuja tu kupitia uhusiano wa binafsi na Mungu, kupitia Yesu Kristo ilituweze kusikia sauti yake ikinena nasi na tutii ambacho anatuambia kufanya. Imani inaleta ufanisi, kwa njia hii iwapo tutakuwa waaminifu katika kweli ya injili, na kuendelea kuamini ndani ya mioyo yetu mpaka mwisho wa maisha yetu hapa duniani.

Je, itakuwaje kuhusu mtu ambaye hana uwezo wa kufanya kazi yeyote kwa sababu ya ulemavu mkali? Jibu ni rahisi sana na la ajabu. Kinachochochea kwa wokovu wetu ni uhusiano na Mungu, yeyote aliye na uhusiano wa kweli na Mungu hata ingawa hawezi akafanya kazi yoyote, uhusiano wao na Mungu kupitia Yesu Kristo ndio wanaohitaji kwa ajili ya wokovu.

Utayari wa injili ya amani

The shoes of the gospel of peace

Kwa wakati mwingi mwanadamu amejaribu kuleta amani katika hali zilioharibika, na amepata kila mara kuwa amani hiyo haidumu. Wakati kutakuwa na amani ya kudumu na amani ya kweli, kila mahali dunuani ni wakati tutapokea kweli ya injli na wajipeane wenyewe katika maisha ya kuabudu na kutii Masihi wa kweli, Yesu Kristo, mwana wa Mungu. Hakuna mwanadamu anayeweza kuleta amani, ni kutawala kwa Yesu tu na kutamaraki diniani milele.

Kuhani wa Mungu katika siku za Musa alipakwa mafuta katika sikio la kulia, mkono wa kulia na mguu wa kulia. Sikio ili kwamba mtu huyo asizikize uvumi mbaya, mambo ambayo sio kweli ya kabisa, ambayo yanaweza leta madhara makumbwa kama vile kuzungumzia kutokuwa mwaminifu kwa Mungu, mkono iliyote atakayoweka mkono wake juu yake yatakuwa kwa heshima na kwa utukufu wa Mungu, na mguuni iliasiende popote ambapo Mungu alikuwa amemwonya asiende.

Mambo yote yalifanywa katika sehemu ya kulia ya mwili, kama ukamilifu wa ishara ya utakatifu. Katika siku za Musa na Wafalme wa Israeli, walipoenda vitani kupigana na adui, kutakuwa na vigingi uwajani vifupi ilikutega, na kuangusha jeshi wanalopigana nalo wanapoendelea, Hivyo hivyo shetani anaweza kukutega iliuingie mahali ambapo Mungu ajakuruhusu wewe kuingia. Iwapo utaingia, basi itakuwa kama kuingia mtegoni, na katika kila hali shetani atakuwa anamaanisha ilikujeruhi.

Chepeo ya Wokovu

The helmet of salvation

Kawaida hii ilikusudiwa iweze kulinda kichwa, lakini katika mambo ya kiroho inazungumzia kile tumelekezea akili zetu, nini tuna tazama, nini tunasoma na ni nini tunawaza. Adui atajaribu kujaza akili zetu kwa vitu ambavyo vinadhuru hata hatari, lakini lazima tujifunze kupambanua kilicho cha Mungu na kisicho cha Mungu. Kuangalia au kusoma kala za ngono, kusoma nyota,kusoma viganja, kusoma majani chai n.k yote ni mambo yale ambao Mungu anatuonya tuweze kujitenga nayo, pamoja na mambo mengine mengi kama vile madawa ya kiasili, matibabu ya sindano pamoja na mengine yaitwayo tiba za kiasili na virutumbusho.

Mtume Paulo akasema kuwa "Iwapo yeyote atakuja kwenu na injili tofauti na ile tuliyoleta kwenu, msiwe na neno lolote na mtu huyo". Tambua anasema "usiwe na neno lolote na mtu huyo" na "usijifunze anacho kuambia iliuweze kumwelezea anapokosea". Iwapoutaelewa injili ya Yesu Kristo inavyostahili, utatambua mara tu anakuja kwako na ya uongo. Mafindisho haya yametayarishwa iliyaweze kukufundisha kweli iliusiweze kupotoshwa na mafundisho ya uongo.

Lazima tuwewangalifu ilitusizijaze akili zetu, na vitu kinyume, na ambavyo viko kinyume na imani. Imani ya kweli ni kufikilia sawa kusudi la Mungu la maisha yako, na mambo ambayo amekuitia kufanya. Iwapo hatutaruhusu mawazo yalio kinyume kuingia akilini mwetu basi sio rahisi kushindwa na mambo yaliyo kinyume. "Yeye aliyekuita ni mwaminifu, naye ataikamilisha."

Darii ya haki

The breastplate of righteousness

Moja ya mambo yaliyo msababisha Yesu kufanya miujiza mingi duniani ni kuwa alikuwa mtu mkamilifu. Hakuwahi kundanganya, hakufanya chochote kwania mbaya na hakutenda dhambi katika sili Akiamini hataonekana. Watu ambao hufanya hivyo kila wakati huwekwa wazi bude au baadaye, haijalishi ni akina nani.

Kwa sababu alikuwa maakini kuendea njia zilizowekwa mbele yake, kama vile hakuna dhambi iliyo patikana ndani yake, aliponena, alichonena kilibeba uzito wa kiroho na mamlaka, kwakuwa hakuwa na uongo ndani yake. Sawa nasi iwapo tutakuwa na uhusiano na Mungu na katika kweli kutofanya chochote ambacho Mungu hawezi akakubaliana nacho, basi nguvu na mamlaka vitakavyokuwa kwa ajili yetu vitakuwa zaidi ya vile vilivyokuwa

Hii ndio sababu makanisa mengi ulimwenguni hayaoni nguvu za kutenda miujiza za Mungu katikati yao, kwa sababu wameenda mbali na viwango na maagizo yaliyowekwa na Mungu kwa watu wa mungu waende jinsi Yesu alivyoenda, katika ushindi mkuu. kama ilivyo na kanisa, ndivyo ilivyo na wakristo binafsi. Tunavyozidi kujiweka mbali na dhambi, ndivyo tunazidi kuishi maisha yanayonyesha nguvu na utukufu wa yule mmoja Mungu aishiye pekee.

Ngao ya imani

The shield of faith

Je, unaamini kile ambacho bibilia inasema kuhusu Yesu na ahadi ambazo ametoa katika neno lake kwako mwenyewe na wote wamfuatao? Unaamini katika Jina lake, una nguvu kinyume na nguvu zote za adui, na pia unaweza kuponya wagonjwa, na kutoa mapepo kwa jina la Yesu? Watu wengi wanakosa kuelewa andiko hilo, halikupi mamlaka ya kuenda kila mahali na kufanya utakavyo, Yesu alifanya tu kile ambacho aliona Baba akifanya.

Muhimu ni kufanya katika amri na sio kutoka kwa akili yako mwenyewe. Hii ni pamoja na kusikia sauti ya Mungu na kuitii, na sio kufanya mpaka umesikia kutoka kwa Mungu, kile unachostahili kufanya katika kila hali. Iwapo utakutana na mtu ampaye anamepagawa, iwapo kazi ya mapepo inatatiza kuhubiri injili, au kuabudu Mungu, una mamlaka ya kuteka nyala pepo hilo na kuliamlisha kutoleta vizuizi. Isipokuwa mtu huyo amekubali ikemewe na apokee Yesu kama mwokozi , hauna uwezo juu yake. Iwapo mtu amekubali Yesu kama mwokozi, una mamlaka kuikemea itoke, lakini unaweza kupewa changamoto na pepo hiyo iwapo kuna shaka akilini mwako kuhusu nguvu na mamlaka uliyonayo ndani ya Yesu Kristo. Shikilia msingi wako kwa ujasiri katika ushindi wa mamlaka yaliyoletwa na Mungu, na haitakuwa na budi ilakuondoka.

Imeonyeshwa hapo mbeleni katika ufupi wa silaha zote za Mungu, iwapouna dhambi za makusudi, ambazo ujakili katika maisha yako, basi nguvu zako na mamlaka yako ndani ya Mungu yatapotea. Katika hali zote kwanza kufunga na maombi yanastahili kutiliwa mkaso. Pia iwapoutajua mapema kuwa utaenda kuwa hudumia wagonjwa, na waliopagaliwa kama juma moja kabla basi leta kanisa lako (pamoja na wewe) kuombea Roho ya uponyaji na ukombozi ilikuwa katika mkutanoni. Wakati mwingi watu huponywa wakati wa kusifu na kuabudu, na kuhubiri neno bila mtu yeyote kuwaguza au kuwakaribia wao. Hapo ndipo utajua kuwa Mungu yuko kazini katikati yenu.

Katika njia nyingine nyingi nguvu zako zitakuja kupitia kuamini kwako, na kusimama katika neno la Mungu. Hakikisha unasoma neno kila siku na utakuwa na ujasiri, kwa kile utakachofanya na kusema. Iwapo utaamlisha mtu aponywe na uwe na shaka moyoni mwako la hili kutendeka, haliwezi kutendeka kabisa.

Iwapo Mungu anafanya kazi ya uponyaji katika mkutano, na uwaombee watu na kuamlisha waponywe, iwapo utakili kwa ujasiri na msukumo basi lazima watapona. Kila wakati kumbuka hizi ndizo taratibu inategemea na Mungu wala sio wewe. Anaweza endelea na afanye mambo makuu hata hivyo.

Upanga wa Roho

The sword of The Spirit

Hili ni neno la Mungu, ambalo limekusundiwa kutumika katika njia ya mpangilio. Unaponena neno la Mungu, kutoka kwenye bibilia an unabii au ujumbe, nena kwa msukumo, kwa sababu kuna mamlaka mengi na nguvu katika kunena neno la Mungu.

Ulimwengu wote uliumbwa kwa neno la Mungu lililonenwa, bado lina nguvu za kubadilisha maisha ya watu, iwapo tutalitumia kwa njia ambayo lilikusudiwa kutumika. Hakuna kutenda kwa akili zetu wenyewe, lakini kutoka kwa amri ya Mungu. Bibilia nyingine zinapendekeza kuwa "maombi yote" au "kuomba katika hali tofauti ndani ya Roho" pia ni silaha ya Mungu, lakini somo hili limewekwa katika sehemu nyingine.

vipawa vya Rohoni kwa ufupi

Summary of Spiritual Gifts "Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika , kama sina upendo nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao Tena nijakuwa na unabii, na kujuasiri zote na maalifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi chakuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwa lisha masikini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sana upendo, hainifaidi kitu." Kwa njia nyingine kifungu hiki kutoka 1Wakorintho sura ya 13 kina hitimisha mambo yote.

Kwa kweli kuna wale ambao wakati wamepokea kipawa cha lugha wanadhani wamefika, na hakuna chochote zaidi cha kulenga tena. Kwa huzuni wao kupokea kipawa hiki na kimekusudiwa kuwa mwanzo tu. Lugha ni kipawa cha lugha ya maombi cha kutumiwa kuchochea uhusiano wako wa ndani na muumba wako, na kutumika kama silaha ya rohoni wakati wa vita vya kiroho na maombezi.

Kuna wale wanaodhani kuwa wao ni wa kiroho sana kuliko yule asiyenena kwa lugha, na basi atatafuta nafasi ya kuonyesha kipawa hiki ambacho Mungu amempatia yeye. Warumi sura ya 8 msitari wa 26 unasema kama ifuatavyo: "kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu: kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo: lakini Roho mwenyewe utuombea kwa kugua kisikoweza kutamkwa."

Paulo anatushauri katika Waefeso 6 "Tuombe ndani ya Roho katika kila hali inavyowezekana." Hii ina maanisha zaidi ya kitu kimoja, ina maanisha kuomba kama vile Mungu ameongoza, kwa lugha ambayo amekupa kwa kusudi hilo. Ina maanisha unaweza kumfanyia mtu maombezi na / au uombe kwa matokeo makubwa. Kuzungumza kwa jumla, kipawa hiki ni cha kutumia katika matumizi yako ya binafsi, na kisitumike kwa umati iwapo hakuna mtu anayeweza kutafsiri.

Kutafsiri lugha

Interpretation of tongues

Wakati mwingine mkutanoni kutakuwa na mtu ambaye atanena kitu Fulani mbele ya umati, kwa luhga tofauti. Wakati mwingi ni maombi ya binafsi au ujumbe kutoka kwa Bwana. Ikiwa sio cha muda wa kipekee kinastahili kitafsiriwe wakati wote na mtu. Kumekuwako na watu mkutanoni ambao hawajaokoka na mtu akanena kwa ujasiri ujumbe kwa lugha ambayo kwa uwezekano hawakuwa wakejifunza – lugha yao wenyewe – hiyo ni kusema lugha ya wageni.

Ingawa kila mtu yeyote, watahitajika kujua kwa lugha yao wenyewe kile ambacho kimesemwa, wageni wanafahamu sawa sawa na wanashangazwa, na kudhihilishwa kwa uwepo wa Mungu katika mkutano. Kutojua kwingine ampako hutokea kila mara ni kuwa tafsiri sio tafsiri ya lugha fulani; kwa hivyo tafsiri yenyewe inaweza kuwa mpango mkumbwa yenye imani zaidi ya ujumbe halisi.

Wakati mwingine itakuwa ni ujumbe wa unabii ambao kanisa linastahili kusikia, katika wakati mwingine itakuwa maombi-ya moyoni ya mtu ambaye amenena. Wengi wameuliza iliwezekana vipi walisikia injili kwa lugha yao ya nyumbani katika siku ya Pentekoste? Muujiza ulikuwa kwa wasikiaji au kwa wanenaji? Tafsiri ya kwanza ya lugha ambayo

mwanafunzi alitoa ilikuwa kutoka kwa mtu aliyenena lugha isiyojulikana na kiongozi wa mkutano akauliza iwapo pana mtu aliye na tafsiri.

Hii hata hivyo ikamchanganya mwanafunzi kama alivyoisikia kwa kingereza kikamilifu, ambicho alikuwa amesikia wakati wote, na kwa bahati zuri alikuwa na ujasiri wakutosha kunena alichosikia, na basi akabariki mkutano kwa neno la kutia moyo kutoka kwa Bwana. Kipawa cha kutafsiri lugha kinaenda pamoja katika wakati mwingi na kipawa cha kutafsiri maono, na kimepokewa na wakristo wengine ndugu na akina dada katika Yesu na kuletwa mkutanoni.

Danieli alikuwa mtafsiri mzuri wa maono kama alivyokuwa Yusufu, kitu cha kushangaza kuhusu Danieli ilikuwa kwamba alipeana tafsiri lakini hakuna yeyote aliyekuwa ame mwambia maono yalivyokuwa. Hii hadithi inawezapatikana katika sura ya 2 msitari wa 14 hadi 28 inasema kama ifuatavyo: "Ndipo Danieli kwa busara na hadhari akamjibu Arioko akida wa walinzi wa mfalme, a liyekuwa ametoka ilikuwauwa wenye hekima wa Babeli: Alijibu akamwambia Alioko, akida wa walinzi wa mfalme, mbona amri hii ya mfalme ni kali namna hii?

Kisha Arioko akamwarifu Danieli habari ile. Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atampa tafsiri ile mfalme. Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari akina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake: iliwaombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli.

Ndipo Danieli akafunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni: Danieli akajibu akasema, na lihimidiwe jina la Mungu milele: kwakuwa hekima na uweza ni wake: Yeye hubadili majira na nyakati: huzulu wafalme na kuwa milikisha wafalme, huwapa hekima wenye hekima: huwapa wenye ufahamu maarifa:

Hufunua mambo ya fumbo na siri: huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake. Nakushukuru na kukuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliotaka kwako, maana umetujulisha neno lile la mfalme.

Basi Danieli akaenda kwa Arioko, aliyewekwa na mfalme kuwaangamiza wenye hekima wa Babel: ailikwenda akamwambia hivi, usiwangamize wenye hekima wa Babeli; niingize mimi mbele ya mfalme, nami nitamwonyesha mfalme ile tafsiri.

Ndipo Arioko akamwingiza Danieli kwa mfalme kwa haraka, akamwambia hivi nimemwona mtu wa hao wana wa Yuda waliohamishwa, atakayemjurisha mfalme ile tafsiri. Mfalme akajibu akamwambia Danieli aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona na tafsiri yake?

Danieli akajibu mbele ya mfalme, akasema ale siri aliyo uliza mfalme, wenye hekima hawa wezi kumfunulia mfalme, wala wachawi wala waganga, wala wanajimu: Lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayo kuwa siku za mwisho"

Katika Yoeli sura ya 2 Mungu anaahidi kuwa ndoto na maono yatakuwa kawaida nyakati zinapokaribia. Yoeli 2 msitari wa 28 na 29 ina sema kwa wazi: "Hata itakuwa baada hayo, ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu waume kwa wake watatabiri, wazee wenu wataona ndoto na vijana wenu wataona maono tena juu ya watumishi wenu wanaume kwa wanawake katika siku zile nitamimina Roho yangu

Labda unashangaa nini tofauti iliyoko kati ya ndoto na maono, jibu ni rahisi, Ndoto ni kitu ambacho unapokea wakati umelala maono ni kitu ambacho unapokea wakati huja lala yote yako katika mchoro na wakati wote katika rangi.

Utambuzi

Discernment

Hiki kipawa kinakuwezesha kukuambia ambacho kinasemwa, au kilicho semwa kimetoka kwa Mungu au nicha mwili. Nikipawa ambacho kinahitajika sana kanisani siku za leo, kwakuwa kina husiana pia na kuwa na ufahamu wa kiroho, wakati kuna mtu mkutanoni anayehitaji ukombozi. Sio kila mtu ambaye amekuja kanisani yupo hapo kwa sababu wanataka kujua zaidi kuhusu Mungu. Wakati mwinguine watakuja na nia ya kuvuruga mkutano, wakati mwingine hii inaweza fanyika bila wao kusema neno au kufanya kelele.

Iwapo roho ya kimapepo iko ndani ya mtu inaweza ikashawishi waliokusanyika, inawezafanya kusifu na kuabudu kuwangumu na katika hali zingine kutowezekana kabisa. Wakati unajua ninani na mahali walipo mkutanoni je, utafanya nini? Hauna ruhusa ya kumwambia aondoke na kiongozi wa mkutano hana kipawa hiki hata kuungamkono hata iwapo utafanya hivyo.

Kwa hakika suruhisho ni kuja pamoja na mtu mwingine mkutanoni, mtu ambaye ni mshilika wa kanisa anayeenda pamoja na Bwana ambaye anajua kuhusu kipawa cha utambuzi na kuomba labda kuwe na kujidhihirisha na pepo kuondoka kupitia kukemewa au mtu anayeshababisha shida aondoke na tuweze kuendelea na mkutano. Wakati mmoja hili lilitokea, Maombi yaliombwa babadaye na baada ya dakika tano mtu mwenye kosa aliamka nakuondoka. Baada ya hilo sifa na kuabudu katika mkutano zikaendelea na uwepo wa Mungu ukasikiwa na wote.

Neno la maarifa

The word of Knowledge

Hii ni uwezo wa kuomba kwa jambo ambalo lime sababisha shida, iwapo unaomba na mtu, au uwezo wa kujua kuwa kuna mtu katika mkutano ana shida Fulani, na kuwa Mungu anataka kumhudumia mtu huyo au watu hao usiku huo.

Unaweza kuonyeshwa mtu mmoja tu mwenye hiyo shida na ushangazwe kuona sita au tano wakitokea kwa huo mwito. Hii haimanishi ulikosea katika kuwaza kuwa alikuwa tu mmoja, inamaanisha kuwa Mungu ana wakati ulioamriwa kwa mtu mmoja katika mkutano huo, lakini kama vile wengine wamejibu kwa imani Mungu atawapa mguzo kutoka kwake pia.

Wakati mwingine ni shida ya kimatibabu, wakati mwingi ni shida ya kihisia, na wakati mwingine ni shida ya kifamilia ambayo inahitaji kushughulikiwa katika siri badala ya faraghani. Iwapo unania na kwa uwazi kufanya kile Mungu anataka wewe ufanye, basi kuwa mwelevu kufuata maagizo. Kipawa hiki ni kwa utukufu wa Jina lake takatifu, sio kipawa kwa njia yeyote kikutukuze wewe.

Uponyaji

Healing

Wakati mwingine Mungu anatutaka tuweke mikono yetu juu ya watu iliawapone, wakati mwingine atafanya kwa ukuu wakati wa sifa na kuabudu. Sio kila mtu atakayekuwa na kipawa moja cha hivi, lakini kwa wakati mmoja ambao Mungu anachagua, na muumini yeyote aliyezaliwa mara yapili anaweza kutumika kwa njia hii.

Unastahili hata hivyo kukumbuka kusonga kwenye mwelekeo wa Mungu, basi katika imani wala sio kwa akili zako. Yesu hakuwahi kwenda kwa akili zake mwenyewe, ni katika amri ya Baba, iwapo kanisa leo lingesoma funzo hili. Watu wengi wameshangazwa na neno la Luka sura ya 5 msitari wa 17 inaposema: "Naikatukia siku moja alipokuwa akifundisha kuwa kulikuwa na mafarisayo na matibabu, wameketi waliokuwa wametoka katika kila mji ndani ya Galilaya, na Yudea, na Yerusalemu: na nguvu za Mungu zilikuwako ili kuwaponya wao."

(Hii bila shaka inamwonyesha Yesu na nguvu za Mungu zakiwapo pamoja naye ili kuponya) kwa njia ambayo msitari huu umeandikwa unaonyesha kuwa hii haikuwa ni jambo la kawaida. Hii inaleta pamoja kikamilifu maneno ya Yesu kwa wanafunzi wake katika Yohana

Sura ya 5 msitari wa 19 inasema: "Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo mwana vile vile." Utajuaje wakati Mungu anasonga na kutaka kuwaponya wagonjwa? kwa utambuzi utambuzi.

Hekima

Wisdom

Kama kipawa cha Rohoni, hii haihusiani na hekima ya dunia kutokana na kupitia mambo au kufanya uamuzi unao hatalisha, hii ni hekima ya Mungu kabisa. Ni kama neno la maarifa au neno la kiunabii, inakujia kwa njia ambayo utakili kwamba sio ya kawaida. Unaweza kuwa hauna chochote akilini mwako – haufikilii chochote – Kisha kwa ghafla Bwana anaweka neno moyoni mwako vile utakavyo kabiliana na hali unayohitaji hekima kwa ajili yake.

Yakobo sura ya 1 msitari wa 5 hadi 8 inasema ifuatavyo na ina husika sana na kipawa hiki: "lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote kwa ukalimu, wala hakemei naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yeyote, maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kuchukuliwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapata kitu kwa Bwana. Mtu wania mbili husitasita katika njia zake zote."

Imani

Faith

Kuna tofauti kumbwa sana kati ya imani na fikira ya matarajio. Imani huja kupitia kisikia, kusikia neno la Mungu. Iwapo unafanya kitu ambacho hujaambiwa na Mungu ufanye basi unafanya kutokana na akili zako mwenyewe wala sio imani. Kipawa cha imani ni wakati utakutana na hali, kitu ambacho kinahitaji ushauri au maombi kwa ajili ya uponyaji, na hapo hapo unakuwa na ushawishi wa asilimia mia unajua ni nini Mungu anaenda kufanya bila kufikiria unakitamka.

Huwezi ukawa na imani hiyo kila wakati ya kuamini hivyo, lakini hii ndio maana kipawa hicho kisicho cha kawaida kinahitajika katika hali nyingi, ili kwamba majibu yako kwa msukumo wa uvuvio wa Mungu, kujua ya kwamba yale ambayo uliyaongea yatakuja kutimia.

Kipawa cha miujiza

Gift of miracles

Hiki ni kipawa ambacho watu wachache sana wakonacho, na inafaa ujue ya kwamba wanapotumia kipawa hiki kwamba Mungu ndiye anayeifanya miujiza, kawaida utaweza kutambua hili kupitia kuhubiriwa neno au kupitia kipawa cha Roho cha utambuzi.

Lakini kumbuka ya kwamba katika ufunuo 13 msitari wa13-14 tunasoma haya kumhusu shetani mwenyewe akiwa anaachiliwa kuongoza ulimwengu kwa miezi 42: "Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu, naye akawa wakoshesha wale wakaao juu ya inchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama akiwaambia wakaao juu ya inchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaiishi."

Basi sasa kwa ufupi na kwa haraka tuangalie juu ya vipawa vya-huduma tano kila kimoja kikiwa kimetengwa na kupewa maelezo ambayo unaweza kuyatarajia kutoka kwa mtu aliyena kipawa hicho.

Mtume

Apostle

Katika maandiko kuna majina tofauti ya kipawa hiki cha huduma, lakini vipawa vyote vya huduma vina kitu kimoja pamoja. Mtume (wakati mwingine anaitwa msimamizi na semazi) ni yule anayezunguka (anapohitajika) akianzisha makanisa mapya, na kuwa mshauri wa kiroho kwa makanisa mengi wakati mwingine duniani kote

Mitume

Prophet

Mpaka kufikia wakati wa Samueli huduma hii ilikuwa inajulikana kama mwonaji, kwa sababu mtu huyo alikuwa anapewa maono ya mambo mengi tofauti. Baadaye akajulikana kama Nabii kwa sababu kazi kuu ya mtu aliye na huduma hii ni kutangaza neno la Mungu, umuhimu sio kutabiri mambo yajayo, ingawaje haiwezi kuepukika kulingana na neno analolipokea kutoka kwa Mungu. Mtu yeyote anaweza kutabiri katika mkutano kwa muda mfupi, lakini yule aliye na huduma ya Nabii atakuwa anatembea katika uwepo wa Mungu, na yuko tayari wakati wote kuleta neno kutoka kwa kiti cha Mungu (kuhubiri) hata kama hakupewa kabisa muda wa kujitayarisha.

Muinjilisti

Evangelist

Kunakutoelewa sana kuhusu huduma ya Muinjilisti. Kazi ya Muinjilisti, sio tu kuleta watu kwa Bwana, kama vile tutakavyoangalia baadaye. Kazi yake, kama kazi yote ya wale walio na vipawa vya huduma-tano ni kutia moyo mwili, na kutayarisha wao kwa kuwafundisha wao vile wanavyoweza kufua nafsi kwa Bwana pia.

Mchungaji

Pastor

Kazi ya Muchungaji kwa ufafanuzi ni kutuza kondoo. Yesu mwenyewe alijiita Mchungaji Mwema, na basi kujitenga na wachungaji wabaya waliotajwa katika Ezekieli sura ya 34. Itakuwa vyema kuangalia sura hii kwa wakati wako binafsi kuangalia ni nini mchungaji ahistahili kufanya, hata kama kuna wachungaji ambao wameshindwa kabisa kutunza kondoo, watahitajika kujibu mbele ya Mungu. Lifanye jambo la furaha mchungaji wako kuwa juu yako katika Bwana, atakuwa na mzigo unaostahili mbila wewe kufanya mambo kuwa magumu kwake.

Mwalimu

Teacher

Wachungaji wengine ni waalimu wazuri sana, walimu wengine wanakua wachungaji wazuri sana, wakati mwingi vipawa hivi vya Huduma haviwezi kumilikiwa na mtu mmoja. Kuna matukio nadra vimeweza, lakini kwa jumla hivi sivyo inavyokuwa. Kazi ya mwalimu ni kutangaza maandiko na neno la Mungu ambalo limetoka katika kiti cha Mungu kwa siku hiyo kwa njia ambayo inaweza kueleweka kwa msikiaji hata wakati hawakupata kitu kama masomo ya ziada ya bibilia.

Kazi yao ni kujua ni nini Mungu anataka kuwafundisha watu kwa wakati Fulani, asichukue somo na aaze kufundisha kwa sababu anafikiria ni zuri kuizungumzia katika siku Fulani.

Iwapo atafanya hivyo hatakuwa hakufundisha tu, lakini atakuwa anafanya pasipo kuruhusiwa na Mungu.

Kazi yo yote ya hawa wamiliki wa Vipawa vya Huduma ni kujenga, kutia moyo na kutayarisha mwili wa Kristo. Katika Wefeso sura ya 4 msitari 11 hadi 13 yote inasema ifuatavyo: "Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa waalimu: kwa kusudi la kuwa kamilisha watakatifu, na ha kazi ya huduma itendeke, na hata mwili wa Kristo ujengwe: hata na sisi siote tutakapo ufikia umoja wa imani na kumfahamu sana mwana wa Mungu, hata kwa mtu mkamilifu, hata kufika kwa cheo ukamilifu wa Kristo:"

Itakuwa ajabu sana kutayasrisha askari kwa silaha za ghalama kubwa, isipokuwa anaenda kutumika wakati huo kwa mabambano. Hivyo hivyo vipawa hivi ni vya kutayarisha watu wa Mungu kwa huduma wenyewe. Katika 1 wakorintho sura 12 msitari 12 hadi 25 tunasoma: "Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja: vivyohivyo na Kristo. Kwa maana katika Roho mmjoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani, ikiwa tu watumwa au waru huru; nasi sote tuliyweshwa Roho mmoja.

Maana mwili si kiungo kimoja, mbali ni vingi. Mguu ukisema kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je, si wa mwili kwa sababu hiyo? Nasikio likisema mimi si jicho mimi si wa mwili; je, si la mwili kwa sabanu hiyo? Kama mwili wote ukiwa jicho, kuwapi kusikia?

Kama wote ni sikio kiwapi kunusa? Bali Mungu amevitia kila viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka. Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja mwili ungekuwa wapi? Lakini sasa viungo ni vingi ila mwili ni mmoja.

Na jicho haliwezi kuambia mkono, sina haja na wewe; waqla tena kichwa hakiwezi kuambia miguu, sina haja na nyinyi. Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vinahitajiwa zaidi; Navile vingine vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana.

Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa: ilikusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe." Isipokuwa sehemu sote zinafanya jinsi sinastahili utakachokuwa nacho kweli ni mwili mgonjwa. Labda hii ndio sababu makanisa mengi yamekuwa dhaifu?

back to main articles page