Tabia ya Koingozi wa Mungu-Aliyepakwa Mafuta

The Character of a God-Ordained Leader

Kufuzu kwa uongozi kumeonyeshwa na Paulo katika maandiko, hasa katika 1 Timotheo sura ya 3 msitari wa 1 hadi 7 yote na 1 Timotheo 5 msitari wa 17 hadi21. Inasema: "Ni neno la kuaminiwa mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa Askofu awe mtu asiye laumika, mme wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa taratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha, si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; mbali awe mpole, si mtu wakujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto wake katika ustahivu; (yaani mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe atalitunzaje kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya ibilisi.

Tena imempasha kushuhudiwa mema na watu walio nje, iliasianguke katika lawama na mtego wa ibilisi." "Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu, hasha hao wajitabishao na kuhutubu na kufundisha. Kwa maana andiko la sema usimfunge ng’ombe kinywa apurapo nafaka.

Na tena mtenda kazi anastahili ujira wake.Usikubali mashtaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu. Wale wadumuo katika kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope. Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele ya Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka, usifanye neno lolote kwa upendeleo."

Kwa ufupi kile ambacho mistari hii inasema, ni kuwa kila mmoja anastahili kutoa hesabu ya upako wa Mungu ambao unadhihilika maishani mwao, na katika huduma, sio katika msingi wa nini anachojua.

Kuwa hivi itakuwa ni uharibifu, kitu ambacho ulimwengu una utaalam wa kufanya. Hiki ni kitu cha kuepukwa wakati wote iwezakanavyo. Kama sivyo kutakuwa na mgawanyiko mkumbwa katika kanisa ambao umesababishwa na kutoangalia sheria hii.

Zaidi, inasemekana anastahili kuwa na sifa zuri kwa watu wasio na dini, hiyo ni kusema watu wanaoenda kanisani ikipendekeza kuwa wakristo wote wanastahili kuhusika, na kuhudumia wengine kwa njia moja au nyingine, na kufanya kitu ambacho Yesu alifanya, kuwa pamoja na kuanza kuwajua walio wa ulimwengu kusudi nafasi ipatikane ya injili kuhubiriwa kwao wakati wataona jinsi ulivyo mtu wa upendo, na mwenye utu.

Wakati Mama Teresa alienda Calcutta, watu huko (hata wale waliokuwa wagonjwa kabisa) walikuwa na wasiwasi naye, na walikuwa wanafunga macho kila mara alipokuwa akianza kunena injili. Baadaye walipo kuja kufahamu alikuwa hapo awaonyeshe wao wote upendo, na ahudumie wagonjwa walifungua akili zao kwa injili, kwa sababu ya upendo wa ndani, na huduma aliyokuwa anaonyesha kwao, iliyokuwa haijaonekana kwa yeyote miongoni mwao hapo nyumae.

Hili laweza kutokea kwako wakati utakutana na watu ambao wana mawazo ya kidunia, kisha unaweza pata nafasi ya kuwa ambia kweli kuhusu Yesu Kristo. Katika Mathayo sura ya 22 msitari 1 hadi 10 Yesu anaelezea hadithi ya mtu aliyeandaa karamu ya arusi lakini wale aliowaalika wakaanza kutoa sababu sizizo kuwa na msingi kwanini hawataweza kuhudhuria, basi akawaamuru watumwa wake waende kila mahali na wafanye watu kuja karamuni ili nyumba ya arusi iweze kujaa.

Inasema "Ufalme wa mbinguni umefananishwa na mfalme aliyemfanyia mwanawe arusi, akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa waje arusini,nao wakakataa kuja. Akatuma tena watu wengine, akisema wambieni walioalikwa, tazameni nimeandaa karamu yangu ng’ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa: na vyote vime kuwa tayari njooni arusuini.Lakini hawakujari wakaenda zao, mmoja shambani kwake mmoja kwenye biashara yake: nao waliosalia wakawakamata watumwa wake, wakawatenda jeuri na kuwaua.

Basi yule mfalme akaghadhibika: akawapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauwaji wale, akateketeza mji wao. Kisha akawaambia watumwa wake, arusi itayasri lakini wale walioalikwa hawa kustahili. Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni waje harusini. Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waowaona waovu na kwa wema, arusi ikajaa wageni.

Arusi ambayo Yesu alikuwa akiizungumzia ni ya Mwana-kondoo. Wayahudi wote walikuwa wamealikwa, lakini kwa sababu waliasi kinyume na mpango wa Mungu, mlango ulifunguliwa kwa Wayahudi pia. Katika fumbo hili tunaona kuwa watumwa walienda kila mahali ambapo walifikiria ilikuhakikisha kulikuwa na wageni wakutosha kujaza nyumba ya arusi.

Iwapo kanisa lako ni la kiuinjilisti, haimanishi kuwa litahubiri injili wakati wageni watakuja ndani kanisani, lakini lazima limaanishe kuwa ni kanisa ambalo linatoka nje katika mkutano wa hadhara kuwa ambia watu wote au binafsi injili ya kweli ya Yesu Kristo. Ni vigumu kuwa la kiuinjilisti na kukosa kufanya hivi kila wakati: kwa hivyo ni muhimu viongiozi kuhusika sana na nafsi ziliopotea.

Katika Marko sura ya 10 msitari 35 hadi 45 tunasoma kuhusu ombi la wanafunzi walioitwa "wana wa ngurumo" inasema kama ifuatavyo: "Na Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakamwendea, Wakamwambia, mwalimu, twataka utufanyie lolote tutakalokuomba. Akawaambia mwataka ni wafanyie nini? Wakamwaambia utujarie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika utukufu wako. Yesu, akawaambia, hamjui mnaloliomba. Mwaweza kukinywea kikombe, ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo ni batizwao mimi? Wakamwambia twaweza. Yesu akawaambia, kikombe nikinyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo ni batizwao mimi mtabatyizwa. Lakini habari ya kuketi katika mkono wangu wakuume au mkono wa kushoto si langu kuwapa ila wao watapewa waliowekewa tayari.

Hata wale kumi waliposikia wakaanza kuwakasirikia Yakobo naYohana. Yesu akawaita, akawaambia, mwajua kuwa wale wanaohesambiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na watumwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu: bali mtu anayetaka kuwa mkumbwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, na mtu anayetaka kuwa wakwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. Kwa maana mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia kwa wengi."

Kanuni zingine za kuwa kiongozi ziko wazi, kama kutokuwa mtu wa kutumia mvinyo lakini kuwa mtu mkalimu, mpenda watu. Iwapo mtu anaenda kuwa katika uongozi wa kanisa lolote lazima wawe kama mfalme katika hadithi ya karamu ya arusi, na kuwahudumia waliopotea kwa moyo wote. Hakuna yeyote anayeweza kufaulu kuliongoza kanisa kwa njia ya kidunia, lakini lazima washiliki moyo wa Mungu sio tu kwa njia ambayo kanisa litaongozwa, lakini pia kwa moyo wa Mungu kwa nafsi ziliopotea ambao hawajawahi hata kuingia kanisani.

Ni njia ya ulimwengu kuonea na kuraghai watu kimawazo, mpaka kuwafanya wafanye ulicho kuwa unataka wafanye, pia ni njia ya ibilisi, njia ambayo inapaswa kufanywa ni kwa unyenyekevu, na kwa mfano wa huduma ya upendo kwa wengine, sanasana wale walio kanisani. Kwa miaka iliopita kume kuwa na kile kilichojulikana kama "kuchunga kwa uzito" mahali ambapo ikiwa mtu anaonyesha kidogo tu kutokubaliana na uongozi wowote wa kanisa, kuhusu chochote kutoka mbele katika mkutano ujao washilika wataambiwa wasiwasiliane na mtu huyo, mpaka watakapokubaliana na uongozi.

Pia hata hawaruhusiwi kuhudhuria kanisa wakati huu, haijalishi ni mhuduma kwa njia yeyote ile. Hii haitoki kwenye bibilia na sio njia ya Bwana pia, usikubali itokee miongoni mwenu kabisa. Karibu makanisa yote yaliofuata "kuchunga kwa uzito" sasa yamefungwa kwa sababu yalipoteza washilika wengi ilikuwa vigumu kwao kuendelea.

Katika kifungu cha kwanza kilichonukuliwa tunaambiwa kiongozi asiwe na wake zaidi ya mmoja. Kijana ambaye hajaoa asioe zaidi ya mke mmoja. Ni rahisi kumpata mtu aliyetimiza kanuni hizi zote lakini bila mwito wa Mungu katika ofisi hiyo. Unaweza kumpata pia ambaye tabia yake inaonyesha yote yaliotajwa katika kifungu hiki, pamoja na kuwa na upako wa Mungu katika maisha yake lakini hajaoa. Wengi watasema leo kuwa hili hali mwuzuilii kuwa kiongozi Fikiria, mmiliki wa kiwanda amekuwa katika biashara kwa muda mrefu na kufanya faida ya kuridhisha kutoka kwa biashara, kwa kufikia maombi ya wateja kwa bidhaa ambayo kiwanda kinatengeneza. Unafikiria ni nini kitakachotokea iwapo kwa ghafla kiwango cha maombi ya kuhitaji bidha kimeongezeka sana? Je, atawaambia wateja watahitajika kusubiri kwa muda mrefu tena au anahitaji kuajiri wafanyakazi wengine? Wengi wataajiri wafanyakazi wengi na ni vyema.

Sasa fikiria kuhusu Yesu, ambaye anaona mambo mengi kuhusu siku za mwisho kufika kuzaa matunda. Aendelee na watu alionao katika huduma Yake sahi, au aongeze idadi ya watu katika huduma yake, kama vile muda unavyoadimika kwa watu wa dunia?

Hakika kama vile uhitaji unavyoongezeka wa watu kufikiwa, na injili ya kweli ya Yesu Kristo kabla kuchelewa, Anastahili kuwaajiri watu wengi ilikuifanya kazi hii kungaliko na wakati. Kwa sababu muda ni mfupi kabla kunyakuliwa kwa kanisa kuweza kutokea, na wale watakaobakia lazima waishi chini ya utawala wa mtu wa dhambi kwa miezi 42 ya kuzimu duniani,( angalia Ufunuo sura ya 13 msitari wa 5) kitu cha busara kufanya ni kutumia watenda kazi wote anaoweza kupata kama vile mwisho unavyokaribia.

Wasitengwe kuwa viongozi, sanasana iwapo wanatimiza matakwa yote yaliotajwa katika vifungu hivi. na pia wana mwito wa Mungu kwa ofisi husika. Viwango hivyo lazima vitumike kwa mtu yeyote. Yeyoye asiteuliwe katika ofisi ya kanisa kuzingatia na usahihi wa kisiasa.

Kulingana na kijana (ndani ya Kristo lakini si kwa miaka) anaweza kuwa, ana uzoevu wakutosha na ufahamu kutimiza ofisi ya kiongozi anavyohitajika, kwa hivyo ni vyema kuwachunguza na kuwachukuwa kama viongozi wa kesho watakapomjua mwokozi, na kujua maandiko zaidi, na zaidi. Kwa bahati mbaya uwezekano wa kijana kujawa na kiburi, ni mwingi kuliko mtu ambaye amekomaa ndani ya Yesu.

Wakati andiko linazungumzia Semazi au Mzimamizi, linazungumzia Mtume badala ya kiongozi na inafaa kufahamika katika mazingara haya. Ni rahisi kupata viongozi ambao hawajaitwa katika moja ya vipawa vya ofisi ya huduma-tano ya Mtume, Nabii, Mwinjilisti, Mchungaji na Mwalimu.

Tambua kuwa kweli huduma hizi ni tano. Ni rahisi kuwa na Mchungaji ambaye si mwalimu wa bibilia, sawa pia ni rahisi kuwa miongoni mwenu na ambaye kwa njia yeyote hana moyo wa uchungaji, ni adimu sana kupata mtu mwenye uwezo wote na upako ndani ya Mungu.

Kitu cha mwisho bibilia ina zungumzia ni watu wasiopenda fedha. Unaofuata ni mfano halisi wa kile kinachofanyika katika makanisa ya magharibi. Mtu mmoja amehudhuria mikutano yote ya wanakamati, mikutano ya mafunzo na ibada kwa miaka 20.

Wakati wanaambiwa wafanye kitu Fulani wamefanya haraka pasipo kunungunika, wala kulalamika, wamekuwa na furaha kutumika kwa njia yeyote. Baada ya majuma machache kunakuja mtu ambaye amehamia hapo karibu, na hajui kabisa mahitaji ya kanisa, amechagua kushiliki hapo. Anazungumza na mchungaji, anamwambia atakuwa ana mwabudu Mungu katika kusanyiko hili wakati wote sasa. Kisha analipatia kanisa kiwango kingi cha fedha, na baada ya miezi michache anapewa kuwa mwenyekiti wa kamati, na anazungumziwa kwa heshima ya kiwango cha juu na mchungaji. Je, hili lina kukumbusha chochote?

Yakobo sura ya 2 msitari wa 1 hadi 9 inasema ifuatavyo: "Ndugu zangu imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu msiwe nayo kwa kupendelea watu. Maana akiingia katika sinagogi mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri, kasha akaingia na masikini,

mwenye mavasi mambovu: nanyi mkimstahi yule alevaa mavazi mazuri, na kumwaambia yule maskini simama wewe pale, au keti miguuni pangu, Je,hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?

Ndugu zangu wapenzi sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na waridhi wa ufalme aliowaahidia wampendao? Bali ninyi mmevunjia heshima maskini, je, matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu? Hawalitukani lile jina zuri mliloitwa?

Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema. Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakoshaji." Hakikisha kuwa mambo haya hayatokei katika kanisa lako. Mungu anafanya na kila mtu sawasawa na atawahukumu wote katika msingi huo huo, au kwa vitu ambavyo vimetajwa katika kufungu kilichotajwa hapo juu, au hadithi iliotangulia katika somo hili.

Je, unafikiria ni vipi mtu mwaminifu atasikia akiona mambo haya yakiiendelea? Uwezekano ni kuwa hatapandwa na hasira tu, lakini kamati pia itakuwa upande wake. Hakikisha kuwa kanisani mwako hakuna sheria moja ya matajiri na nyingine ya maskini, hakikisha sheria inatumika kwa wote bila kujali kiwango cha fedha zao au itawapa hasira wengi katika kusanyiko pia, hawa wanaweza kuchagua na kwenda kwingine, hii inamaanisha kuwa vipawa vya Rohoni vinapo angaliwa kanisa lako litakuwa maskini zaidi.

Tabia ya kiongozi wa kanisa anastahili kuwa wazi, na anastahili kuwa mtu yule aliyetayari kujadili chochote na yeyote kanisani, iwapo watafikiri kuwa amekosea katika jambo lolote. Mheshimu Yesu kwa njia zote naye atakuheshimu. Mpango alionayo kwa makanisa yote ulimwenguni kote, na yale yatakayoazizwa hivi karibuni, iwapo wewe ni mwanifu kwa Mungu basi atakuhusisha katika mipango hiyo, bora viongozi wote wawe watu wakuomba na wanafunga kila siku, na kuomba iliwaweze kuwa na uwezo zaidi wa kusikia mwuongozo, na maagizo ya Mungu. Siku zijazo zina nuru kubwa lakini kila wakati ni wewe kuitikia katika njia ambayo, Mungu anahitaji kutoka kwa viongozi.

back to main articles page