Ishara za kurudi kwa masihi wa kweli

Signs of the true Messiah’s return

Hesabu sura ya 2 msitari wa 1 hadi 3, inapeana maagizo kwa kabila kumi na mbili jinsi wanastahili kuzunguka hema ya kukutania wakati itakapojengwa. "Bwana akanena na Musa na Haruni na kuwaambia, wana wa Israeli watapanga kila mtu penye beramu yake mwenyewe, na alama za nyumba za baba zao; kuikabili hema ya kukutania ndiko watakapopanga kwa kuizunguka pande zote.

Na hao watakao panga upande wa mashariki, kuelekea mawio ya jua, ndio wale wa beramu ya marago ya Yuda, kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Yuda atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu." Hii inamaanisha hapo mbele ya mlango wa kuingia hema ya kukutania ni kabila la Yuda. Basi yeyote atokaye kastika uwepo wa Bwana ndani ya hema lazima aje kupitia kabila la Yuda.

Vivyo hivyo, wakati Masihi wa kweli atakaporudi kujenga ufalme wake hapa duniani, kwa miaka 1000 ukoo wake lazima uwe unaoweza kufuatiliwa nyuma kupitia kabila la Yuda na hata pia nyuma kufikia Adamu. Wana theologia wengi hudhania wakati masihi wa uongo atakapoonekana, ambaye katika kweli takuwa ni ibilisi amechukua mwili wa mwanadamu basi ukoo wake waweza kufuatiliwa nyuma mpaka kabila la Dani.

Hili basi lafaa liweke hii wazi kwa watu wa Mungu ya kwamba ni masihi wa uongo, na sio yule wa kweli. Hata hivyo katika wakati huu wa siku za mwisho, wengi watandanganyika na kumfuata yeye, kwa kutojua wakimwamini kuwa ndiye waliyekuwa wakimngojea kwa sababu ya miujiza atakayokuwa akifanya katikati yao.

Moja ya ishara hizi au miujiza itakuwa ni kuita moto kutoka mbinguni, kama vile Eliya alifanya katika siku zake. Ufunuo sura ya 13 msitari wa 11 hadi 14, inatupatia ishara nyingine ya kuweza kumtambua masihi wa uongo. "Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi, naye alikuwa na pembe mbili mfano wa mwana-kondoo, akanena kama joka.

Naye atumia uwezo wote wa yule mnyama wa kwanza mbele yake, Naye anaifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Naye afanya ishara kubwa, Hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi."

Tunaona kutoka kwa misitari hii kuwa ana uwezo wa kuita moto kutoka mbinguni, ambayo ni moja ya mambo ambayo Eliya alifanya katika wakati wake, na yameandikwa katika 2 Wafalme sura ya 2 msitari wa 9 hadi 18. "Ndipo mfalme akatuma akida wa askari hamsini pamoja na hamsini wake, wamwendee Eliya, akamwendea na tazama, ameketi juu ya kilima.

Akamwambia, ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, shuka. Eliya akajibu akamwambia, Yule akida wa hamsini, ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako, moto ukashuka ukamteketeza, yeye na hamsini wake. Akatuma tena akida wa hamsini mwingine pamoja na hamsini wake, wamwendee akajibu akamwambia, Ewe mtu wa Mungu mfalme asema shuka upesi. Eliya akajibu, akamwambia, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni ukuteketeze wewe na hamsini wako.

Moto wa Mungu ukashuka kutoka mbinguni, ukamteketeza yeye pamoja na hamsini wake. Tena akatuma akida wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule akida wa hamsini wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini ziwe na thamani machoni pako. Tazama, moto ulitoka mbinguni, ukawateketeza wale akida wawili

wa hamsini wa kwanza pamoja na hamsini wao, laiti sasa roho yangu na iwe na thamani machoni pako.

Malaika wa Bwana akamwambia Eliya, Shuka pamoja naye; usimwogope. Akaondoka, akashuka pamoja naye hata kwa mfalme." Sababu ya kwanza ya kufanywa mujiza huu na masihi wa uongo, ni kwa sababu Wayahudi wanasubiri kurudi kwa Eliya wazi wazi ambaye atamdhihilisha Masihi kwao.

Watu hawa watandanganyika hata kuamini kuwa mtu aliye pamoja na masihi wa uongo ndiye wa kweli, kwa sababu atadhihilishwa na yeye ambaye amepewa kufanya miujiza hiyo ya uongo.

Ishara ya pili ya kuwa huyu ndiye masihi wa uongo, ni kweli kuwa wameamrishwa kufanya sanamu ya mnyama na kuabudu pamoja na mnyama. Hili haliwezi kuamriwa na Masihi wa kweli, kama vile amri moja kati ya zile kumi inasema, hakuna sanamu ya chochote kilicho mbinguni na duniani itakayofanywa, tena mtu yeyote asisujudie na kuabudu yeyote isipokuwa Mungu wa kweli mmoja aishiye na aliyeumba vitu vyote.

Ishara zaidi ya Masihi wa kweli imeandikwa katika Zakaria sura ya 14 msitari wa 1 hadi 4. Hii inasema hivi: "Tazama, siku moja ya Bwana inakuja, ambayo mateka yatagawanyika kati yako. Kwa maana nitawakusanya mataifa yote walete vita juu ya Yerusalemu; na huo mji utapigwa, nazo nyumba zitatekwa, nao wanawake watatendwa jeuri; na nusu ya watu watatoka kwenda utumwani; ila mabaki ya watu wa mji hawatakatiliwa mbali.

Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alivyopigana zamani katika siku ya vita. Na siku hiyo miguu yake itasimama ju ya mlima wa mzeituni unaonekana Yerusalemu upande wa mashariki nao mlima wa mzeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu yam lima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini." hili ndilo Masihi wa kweli anaweza kufanya.

Wasomi wengi wa bibilia wanafikiria kuwa hii ilikuwa ni kumbukumbu ya fumbo, hawakuwa na ufahamu ni vipi Mlima wa Mzeituni unaweza kupasuka katikati kama vile ambavyo imeonyeshwa hapa. Tena pamoja na kuendelea kwa teknolojia katika karne ya ishirini, ilitambuliwa kuwa kuna ufa ambao uko katikati ya Mlima wa Mzeituni unoweza kusababisha mtetemeko, utakaoleta jambo hili kama vile limeonyeshwa katika maandiko.

Masihi wa kweli kushuka juu ya Mlima wa Mzeituni, ni kutimizwa kwa maneno ya malaika kwa wanafunzi wa Yesu alipopaa kwenda mbinguni. Hili limeandikwa katika Matendo sura ya 1 msitari wa 9 hadi 12 inasema: "Akisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.

Walipokuwa wakikasa macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mpona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni. Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima uitwao Mlima wa Mizeituni uliokaribu na Yerusalemu wapata mwendo wa sabato."

Zaidi, katika mazungumzo kuhusu ishara za mwisho Yesu alisema kuwa kurudi kwake hukutakuwa kumesitilika kwa kuwa kutaonekana na watu wote. Mathayo sura ya 24 msitari wa 27 inasema: "Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kujakwake mwana wa Mungu."

Mpaka wakati teknologia ya setelaiti iliweza kuanziswa katika mwisho wa kanre ya ishirini, imekuwa rahisi kila tukio kuonekana na ulimwengu wote kwa wakati huo huo. Mfano wa hivi karibuni kuhusu hili ulikuwa kuja kwa milenia mpya. Katika tukio hilo watu katika mataifa ya magharibi waliweza kuona tukio kubwa ambalo lilikuwa likifanyika katika upande wa mashariki wa ulimwengu wakati lilipokuwa linafanyika.

Kwa karne nyingi wana theologia wengi wamekuwa waking’ang’ana juu ya vifungu viwili, moja katika Agano la Kale nyingine katika Agano Jipya. Iliyo katika Agano Jipya inatoka 2 Petro sura ya 3 na msitari wa 10 inayosema: "Lakini siku ya Bwana itakuwa kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea."

Je, hili lina maanisha nini? Je, litafanyika vipi? Andiko lingine ambalo limewashinda wanatheologia kwa karne nyingi ni kutoka Zakaria sura ya 14 msitari wa 12 inayosema: "Na hii ndiyo tauni, ambayo Bwana atawapiga watu wote waliofanya vita juu ya Yerusalemu:

Nyama na mwili wao itaharibika, wasimamapo juu ya miguu yao, na macho yao yataharibika, ndani ya vichwa vyao, na ndimi zao zitahalibika vinywani mwao." Wakati wa vita vya pili vya dunia kila kitu kilifanywa ili kuzuia Nazis kuteka ulimwengu.

Silaha za kupigana vita zilikuwa zina buniwa haraka ajabu. Teknologia ya roketi ikazaliwa, na ikawekwa siri kwa wote, lakini mafunzo machache yalikuwa yanaendelea, kutengeneza ambayo ni silaha yenye maangamizi kuliko zote ambazo zinajulikana na mwanadamu. Ni silaha ya niukilia iliyoangushwa juu ya Hiroshima.

Matokeo ya kukabiliwa na bomu hii ikawa watu hawa waliokuwa maeneo ya wazi, miili yao iliungua wakiwa wamesimama kwa miguu yao na macho yao yakayeyuka katika soketi zao. Utabiri wa ajabu wa tukio la zaidi ya miaka 2000 katika siku zijazo limetukia. Bila shaka hili ndilo Zakaria alikuwa akielezea. Kwa zana za nukilia vitu huyeyuka ndani ya joto.

Ingawa waliishi miaka mamia mbali mbali, sasa tunajua Petro na Zakaria walikuwa wa wanaelezea jambo moja, silaha ya nukilia ambayo haikuwa imefumbuliwa hadi karibu katikati ya mwaka wa 1940.

Katika Mathayo sura ya 24 msitari wa 32 hadi 34 tunasoma: "Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua kuwa wakati wa mavuno u karibu; nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.

Amini, na wambia, kizazi hiki hakitapita, hata yote yatakapotimia." Ni kizazi kipi? Ni kazazi cha wale wanaoishi wakati mambo haya yanapotukia."

Mstari wa 32 unazungumzia kuhusu kuchanua kwa mtini, na Yesu anasema wakati unaanza kuchanua mnajua kuwa mmekaribia wakati wa mavuno. Katika mwaka wa 1948 Israeli kwa mara nyingine ikawa taifa, na kwa nembo ya taifa lao wakachagua …..mtini. Hili laweza kuwa jambo la kawaida lakini zaidi laweza kuwa ni kutimia kwa lile ambalo Yesu alikuwa akizungumza katika misitari hii.

Katika Ufunuo sura ya 9 msitari wa 16, Yohana aliona jeshi kubwa sana, hesabu ya majeshi wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao. Katika siku yake hesabu hiyo ya watu ilikuwa haiwezi kuopatikana ulimwenguni, lakini sasa Japani likiwa sio taifa lisilo na jeshi tena na China ikiwa na jeshi kubwa basi ni rahisi sasa kwa jeshi kubwa kiasi hicho kusimama kinyume, mambo haya yote yamefanyika katika nusu ya karne ya ishirini.

Jambo la kufurahisha ni kuwa iwapo utatazama katika Ufunuo sura ya 19 msitari wa 6 hadi 11, tunasoma: "Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki. Natufurahi tushangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya mwana-kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. Naye akaniambia, andika, heri walioalikwa, karamu ya mwana-kondoo. Akaniambia, maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu. Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie,

Akaniambia, wacha usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe,

nayeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-Kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita."

Watu ambao wanaenda kuwa katika Karamu ya Arusi ya Mwana-kondoo, ni waumini waliozaliwa mara ya pili, waliopeana maisha yao kwa Yesu wakati ambao walikuwa hai. Hilo linamaanisha kuwa iwapo tutachukulia yale ambayo yameandikwa, kuwa yako katika taratibu ya kutimia, hakuna sababu ya kuamini mambo njia tofauti, tutashiriki katika Arusi ya Karamu ya Mwana-kondoo mbinguni ingawa vita vya kwanza vya mwisho vinaendelea.

Kwa siri miaka ya 1970 Urusi ilijaribu kupiga Israeli kwa njia ambayo imeonyeshwa, lakini wakati wakufanyika kama vile imeonyeshwa katika maandiko haukuwa umetimia, naye Mungu akawakatilia mbali kwa mkono wake. Unaweza kuwa na uhakika kuwa watajaribu tena hivi karibuni, hatujui bado ni lini, lakini lazima tuwafikie watu wengi kama iwezekanavyo kwa wakati huu tulionao. Tukiwa na wokovu wetu uliohakikishwa hakuna sababu yeyote sisi kutofanya.

Mathayo sura ya 24 msitari wa 6 na 7, ni mahali pengine ambapo tumeonywa kwa mambo yatakayo kuja. "Nanyi mtasikia habari za vita na matetezi ya vita; angalieni msitishwe, maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali."

Matetemeko yamekuwa yakiendelea kwa maelfu ya miaka, basi kwa nini tunafikilia tunaishi wakati wa mwisho? Jibu ni kwamba matetemeko haya sasa, na majanga yanafanyika katika hali isiyoweza kutambuliwa katika marudio na uzito. Ni mwaka jana tu Marekani ilikumbwa na msimu wa kimbunga ambao haujawahi kuonekana, pamoja na kama kimbunga kiwango 1 kimbunga cha kiwango cha juu 5 kwa msingi wa uharibifu wake.

Tunaona mafuriko mabaya yamefanyika Maine, jimbo liloko katika kusini magharibi mwa Marekani, wakati mto ulipanda kwa mara ya kwanza futi 30. Uropa hivi karibuni imerekondi viwango vya juu vya joto kuliko hapo awali, kilichofuatia punde na mavuliko yaliyosababishwa na uzito wa dhoruba uliofuata wimbi la joto.

Katika disemba 2004 tetemeko katika Bahari ya Hindi ilisababisha Tsunami iliyoleta uharibifu katika sehemu za India, Afrika, Thailand na sehemu nyingi za ulimwengu. Hii ilisababishwa na uzito wa tetemeko ambalo lilikuwa limefanyika katika sehemu iliyoharibiwa maili 600 kutoka kazkazini na kusini – sehemu iliyoharibiwa ni sehemu ya nchi iliyovunjwa na sasa ni dhaifu sana ambayo inauwezekano wakuharibiwa wakati wowote wa hali ya tectonic (mtetemeko wa ardhi).

Kumekuwa na matetemeko mengi ya ardhi katika sehemu hii iliyoharibiwa, hapo awali ikinyakua sehemu chache za upana wakati inatukia, lakini tetemeko la Disemba 26 2004 lilikuwa mbaya sana kiasi cha maili 600 kilinyakuliwa. Hili halijawahi kuwa hapo nyuma katika historia.

Sio hilo pekee lakini tetemeko lilipimwa 9.5 katika Richter kipimo cha kupima kiasi cha tetemeko, kabla ya hili hakuna tetemeko ambalo lilikuwa limepimwa zaidi ya 8.7 basi hili lilikuwa sio la kawaida kabisa.

Kabla ya mwaka mmoja pwani ya Aegean eneo ambalo haliko mbali kutoka Ugiriki, kulikuwa na kile kinachojulikana kama tetemeko la ardhi la dhoruba. Kinachofanyika ni kuwa kunapokuwa na tetemeko la ardhi katika sehemu ya kusini mwa sehemu iliyoharibiwa, kwa wakati huo huo inachochoea kuwa na matetemeko mengine ya ardhi kwa muda Fulani, katika sehemu za kuelekea kaskazini mwa mahali palipo haribika kila wakati. Hili kwa hakika hali kurekodiwa au kujulikana kwazaidi ya miaka 2000.

Kiwango cha majanga, ukame na mafuriko kimeongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka kumi iliyopita, na kiko juu sana leo, yaani badala ya kuwa na musimu mmoja wa janga la maafa mabaya katika miezi kumi na miwili, sasa tuna kiwango cha kama sita. Tena Marekani

wakati mfupi uliopita watu wengi waliuawa na kimbunga kilichofanyika katika sehemu ya Marekani, kimbunga ambacho hakijawahi kuonekana hapo nyuma.

Unaweza sema kwa mawasiliano tuliyonayo katika ulimwengu wa kisasa twawezaje kuwa na habari za vita zikiendelea? Basi sasa hivi katika kijiji kidogo kilicho eneo la Kaskazini mwa China kunadhaniwa kuna mapigano katika mpaka na taifa lingine la Bara Asia, lakini sehemu hiyo ni kijiji kidogo sana na hakuna yeyote amewahi kuenda huko kuhakikisha hili.

Njaa inaonekana leo katika kiwango kikubwa kuliko hapo awali, sana sana eneo la kaskazini mashariki mwa Afrika, lakini hili silo eneo pekee la ulimwengu ambalo lina shuhudia janga mbaya la njaa, inafanyika India na sehemu zingine nyingi za ulimwengu ambazo hazijawahi kuona njaa hapo nyuma.

Hivi karibuni China imekuwa na msimu wa mvua kubwa ambao haujawahi kujulikana hapo nyuma, ikasababisha Bombay kukosa mawasiliano kupitia mabasi, gari moshi na laini za simu (inayo maanisha hakuna umeme basi iwapo mtu ana tarakilishi hapo haiwezi kufanya kazi) ikawa haiwezekani kutembea kwa miguu kwa majuma mengi kwa sababu ya kiwango cha maji ya mafuriko yaliyo sababishwa na mvua kubwa ya ghafla.

Australia sasa hivi inapitia ukame mbaya, na chakula hakipatikani kwa sababu ya kukosa mvua kwa miaka, ili wakulima waweze kupanda mimea au kuwalisha wanyama ambalo laweza kuleta chakula. Katika sehemu zingine za nchi bei ya chakula inaongezeka siku baada ya siku na iko juu sana katika sehemu za Afrika, hata mtu maskini kabisa hawezi akamudu kununua na mataifa tajiri wanaonekana kufungia macho hali hiyo.

Mfumko wa bei Zimbabwe imerekodi rasmi asilimia 1000 kila juma, na maduka mengi yanafungwa, kwa sababu hayana chakula cha kuuza. Hakuna ajuaye hali hii itaendelea hata lini. Mambo haya yanafanyika leo kwa kiwango cha bibilia.

Iwapo utatazama katika maandiko ya Paulo kwa makanisa, sana sana kwa Wathesalanike utaona alishiliki kuwa kurudi kwa Yesu kuko karibu sana. Iwapo alikosea, basi (kama alivyokuwa) kwa nini yeyote afikirie kurudi kwa Yesu Kristo kukokaribu leo? Jibu rahisi kwa hilo swali ni kuwa kitabu cha Ufunuo kiliandikwa miaka 20 baada ya kifo cha Paulo.

Katika kitabu cha Ufunuo sura ya 13 msitari wa 16 hadi 18, Yohana anazungumzia jamii ambayo haina fedha, na hakuna yeyote anayeweza kununua au kuuza chochote isipokuwa ana alama ya mnyama katika kipaji cha uso au katika mkono wa kuume. "Naye (mnyama) awafanya wote wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita sitini na sita.

Wakati Yohana aliyaona maono haya hakuna yeyote aliyejua kuna tekinologia ya tarakilishi, kama vile itachukuwa miaka elfu moja na mia tisa kabla kutimia. Leo tunajua hii nambari ni nambari ya usajiri wa mtu binafsi ambayo inaweza kuchujwa na tarakilishi mahali popote ulipo ulimwenguni, na shughuli zako sote zinaweza kurekodiwa na taraklilishi kupitia kuchujwa kwa microchip

Imejaribiwa Marekani na imekubalika kuwa sehemu muhimu unayoweza kuwa nayo ni katika kipaji cha uso wako, au nyuma ya mkono wako (yaani ndani ya ngozi katika matukio yote) wamemudu teknologia hii na wanyama, na wakati huu sasa kambuni inatimiza agizo lake kutoka kwa serikali ya Uingereza kutengeneza microchip yenye habari za mtu binafsi ndani yake kwa kila mtu ulimwenguni kote.

Unaweza kusema "Lakini hakuna tarakilishi ulimwenguni ambayo inaweza kurekodi shughuli kama hizo kikamilifu, na kwa utosherevu." Ndio ipo, katika moja ya mataifa ya Uingereza kuna taralishi, katika jengo moja ya serikali ambayo ni kubwa sana kiasi cha kujinyosha kama orofa nne za jengo.

Hii inaweza kurekodi shughuli nyingi za kila mtu aliyevaa microchip. Tarakilishi hiyo ni kubwa sana hata inaitwa "Mnyama". Tarakilishi hii iko tayari kuletwa na kutumika wakati wa serikali moja ulimwenguni, mazungumzo ambayo yamekuwa yakiendelea kwa karibu miaka 60 sasa, na yako karibu kukamilika. Kuweka kweli hizi pamoja tunaweza kuhitimiza kwamba hizi ni ishara za kurudi kwake Masihi wa kweli hivi karibuni.

back to main articles page