Sifa na Kuabudu

Praise and worship

Ni nini tunaweza kujifunza kutoka kwa maandiko kuhusu somo hili? Je, kuna kifungu ambacho hasa kina msaada kwa mafunzo yetu katika somo hili? Jibu la maswali haya yote mawili ni sahihi kabisa. Zaburi 100, ina mistari mitano tu lakini inatupa sababu nyingi za kumsifu Mungu tunavyoangalia.

"Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote. Mtumikieni Bwana kwa furaha, njoni mbele zake kwa kuimba. Jueni kuwa Bwana ndiye Mungu: ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake, na kondoo wamalisho yake. Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru: nyuani mwake kwa kusifu: mshukuruni, lihimidini jina lake. Kwa kuwa Bwana ndiye mwema, rehema zake niza milele, na uaminifu wake vizazi na vizazi.

Kwanza, inatuambia sifa zetu kwa Mungu inastahili ziwe sauti ya furaha, na sio kama kitu kinachotoka kwa kusitasita. Wakati mwingine tunapopitia hali ngumu inawezekana kuona, kumsifu Mungu katika hali hizo ni ngumu sana, lakini kuna mistari katika bibilia ambayo inazungumzia hili na inatupatia ushauri katika hali kama hizi.

Tunashauriwa tumpe Mungu shukurani katika hali zote, ingawaje sio kwa hali zote. Wakati tunadumu katika hali zetu badala ya uwezo wa Mungu kuzishida, tuko hatarini kuona shida zikiwa kubwa kuliko Mungu. Wakati tunainua macho yetu kwa Mungu na kuazimia mioyoni mwetu kumsifu katika kweli, tunaona shida zetu na hali zetu katika mtazamo tofauti.

Wahebrania sura ya 13 msitari 15, inakiri kuwa wakati mwingine sadaka zetu za sifa katika hali ngumu zinaweza kuwa sadaka zakujitoa. "Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima yaani tunda la midomo iliungamao jina lake"

Iwapo utatazama kitabu cha Hesabu sura ya 2 msitari 1 hadi 3, Tunaona upande wa mashariki mbele ya kiingilio cha hema ya kukutania ni kabila la Yuda. Hili linafanywa, ilikuwaonyesha watu kuwa Masihi wao wa kweli atakuja kupitia kabila la Yuda. Jina Yuda pia linamaanisha sifa, basi ni wazi kuwa tunapoanza kumsifu Mungu kwa mioyo yetu yote, hili linavuta uwepo wa Mungu na linamfanya yeye rahisi kujionyesha katikati yetu kwa njia inayoonekana na ya nguvu.

Watu wengi wamepokea uponyaji wakati wa sifa na kuabudu katika mkutano, basipo mtu kuwaombea wala kuwawekea mkono kwa njia yeyote. Wakati mwingine utaweza kuona waziwazi mapepo yakijidhihilisha, na kuwatoka watu kwa sababu wanatuchukia tunapomsifu Mungu kutoka kwa mioyo yetu yote.

Sehemu nyingine ya Zaburi inasema, "mtumikieni Bwana kwa furaha" tambua hili, sio kwa kusitasita lakini kwa furaha na kwa hiari, kutoka kwa upendo, na kushukuru kwa mambo yote mema aliyokufanyia. Moja ya makosa ambayo watumwa wa Kihebrania walifanya wakati walipotolewa Misri kwa njia ya kimiujiza, ilikuwa badala ya kumshukuru kwa ukombozi huo wa ajabu, walikuwa wanaendelea kumwombolezea wakati wote, na hawa kuonyesha hata sehemu ndogo ya furaha au kushukuru wakati wowote. Hivyo wakakosa kuingia nchi ambayo Mungu kwa muda mrefu aliahidi kuwapa kuwa yao milele.

Sehemu nyingine ya Zaburi hii inatukumbusha tujue kuwa Bwana ni mwema, na hili pekee lina mfanya kustahili sifa zetu. Wakati aliwaokoa watumwa wa Kihebrania kutoka Misri ilikusudiwa kuwa mfano wa kuonekana, wa kile Masihi atafanya alipokuja, na kuwa ametukomboa na utumwa wa dhambi, na kutufanya sisi rahisi kupatanishwa na kuishi naye milele katika ufalme wake wa mbinguni, kwa mambo haya Anastahili sifa milele na kushukuriwa.

Wakati watumwa wa Kihebrania waliongozwa na Musa jangwani, walikutana na shida karibu kila sehemu, Huyu alikuwa ni Mungu anawajaribu wao ilikuona iwapo walikuwa na moyo wa

kweli, wa kumtegemea na kumtii Yeye au itajukua maisha yao yote kutoa kumbukumbu za Misri, kutoka mioyoni mwao na akilini mwao, ilikwamba wamtazame Mungu aliyewakomboa na kuonyesha kibali chake na baraka zake juu yao kwa matukio mengi.

Sehemu nyinguine ya Zaburi hii inatukumbusha kuwa ni Yeye aliyetuumba. Watu wengi ulimwenguni hujiita waliojitengeneza-wenyewe, watu wanaposhida shida kubwa wapate kufaulu na watu tajiri wanaume na wanawake ulimwenguni. Wanasahasu kuwa hili halingeweza kuwezekana isipokuwa Bwana amewapatia uwezo wa kupata utajiri.

Kuwa mtu tajiri sio dhambi, lakini kile unachofanya na utajiri huo chaweza kuwa. Iwapo utaitumia kuendeleza ufalme wa Mungu duniani basi unaitumia kwa kusudi uliyoipewa, lakini iwapo unakuwa mwenye tamaa kupindukia na mchoyo, basi utalipa, wapenzi milele utakapojibu kwa Mungu nini umefanyia maisha yako hapa duniani.

Tunaweza katika hali hizi tukasahau kuwa Mungu ni Baba yetu, na anataka sana kuwa na ushirika wa ndani nasi. Utajiri unaweza kutupofusha katika kweli hii, na kutufanya sisi kugeuka kutoka Kwake katika nia zetu za ubinafsi mwingi. Kuna vitu katika maandiko ambavyo hata wakristo wachache wanaonekana kuamini kabisa, moja ya haya ni kile Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuhusu kutoa, katika Luka 6 mstari wa 38, Yesu anasema kitu kikubwa kuhusu nini unastahili kufanya na mali yako, haijalishi utajiri wako au umaskini wako.

Mistari hiyo inasema kama ifuatavyo: "Wapeni watu vitu nanyi mtapewa, kipimo cha kujaa na kushidiliwa, na kushukwa-shukwa hata kumwagika, ndicho watu watakacho wapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa." Iwapo tutamruhusu Mungu atakuwa kama mchungaji kwetu, akituongoza sisi hata malisho mema (vitu) ingawaje wakati mwingine inaweza kuonekana kama njia ngumu kabla hatujafika hapo, tutapata kuwa wakati wote baraka hazilingani na njia ngumu.

Katika Yohana sura ya 10 Yesu alisema kama ifuatavyo: "Kondoo wangu wanaiskia sauti yangu, na nina wajua, na wananifuata: ni nawapa uzima wa milele; na hawataangamia, na hakuna yeyote atakaye watoa mkononi mwangu."

Unaweza kusikia sauti ya Mchungaji Mwema Yesu iwapouna uhusiano naye, kwa sababu unapomfanya yeye kuwa mchungaji wako na kiongozi katika maisha yako yote, Atakufundisha kumjua yeye na kutii sauti yake.

Basi tuna maagizo ya ni vipi tunastahili kuingia uweponi mwa Mungu, tunapokuja mbele zake kwa sifa na kuabudu, au wakati wowote. Sehemu ya kwanza ya msitari wa 4 inasema: "Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru, nyuani mwake kwa kusifu." Haipendekezi kuwa tuingie mbele zake tukitarajia kuwa Mungu atatuonea huruma sisi kwa magumu ambayo tunapitia, wakati tunaanza kumshukuru Mungu kwa mambo ya ajabu ambayo ametutendea, anapata kutusikia na anazikiliza maombi yetu.

Kitu kimoja kisicho wezekana kwa mwanadamu na milele kitabaki kuwa hivyo, Mungu amekuwa mwema kwa kutukomboa sisi kutoka kule tulipokuwa tunaelekea kiroho na kimwili, (shimo la jehanamu) na sasa ametugeuza na kufanya rahisi kwetu kuishi pamoja naye mbinguni, pasipo machozi, pasipo na mateso, na pasipo kifo katika milele yote. Kwa mambo haya hatutaweza kumpa shukrani za kutosha na sifa.

Tayari tumeeona vile Bwana alivyo mwema, lakini msitari wa mwisho wa Zaburi 100 unatukumbusha kuwa rehema zake na uaminifu wake ni za milele, Kitu ambacho kiko imara na hakihitaji kubadilishwa, hata hivyo mabandiliko hayo hayatakuwa kwa wema bali kwa hasara.

Wahebrania sura ya 13 msitari wa 8 inatukumbusha kuwa Mungu habadiliki yeye ni yule yule milele yote. Yesu ndiye mwakilishi kamili wa Baba na amefanana naye katika tabia. Wahebrania 13 Inasema: "Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele." Iwapo tunataka kumjua Mungu Baba alivyo basi tunaweza kumwangalia Yesu, Mwana pekee wa Mungu, aliyetungwa mimba na Mungu mwenyewe na kuzaliwa na bikira Mariamu.

Kataka Maombolezo sura ya 3 msitari wa 21 hadi 25 Yeremia anaonyesha wema na rehema za Mungu. "Najikumbusha neno hili, kwa hiyo nina matumaini. Ni huruma za Bwana kwamba hutuangamii, kwakua rehema zake hazikomi. Nimpya kila siku asubuhi: uaminifu wako ni mkuu, Bwana ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, kwa hiyo nitamtumaini yeye, Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, kwa hiyo nafsi imtafutayo."

Katika Zaburi 22 mstari wa 3, inasema: "Bwana wewe umtakatifu, uketiye juu ya sifa za Israeli." Ingawaje msitari huu unasema Bwana anakaa juu ya sifa za Israeli unaweza kuhakikishiwa kuwa ni kweli kusema kuwa Bwana anakaa juu ya sifa za watu wake wote. Kile ambacho Mungu anataka ni kuwa sifa hizi zitoke kwenye moyo mbali sio kutoka kwa kinywa

Mathayo sura ya 15 msitari wa 7, inatukumbusha sisi maneno ya Yesu kuhusu kuabudu kutoka kwa moyo ambapo ndipo mahali ambapo kuabudu kwa kweli kunaweza kutoka: " Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu akisema,watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami."

Alikuwa anazungumzia watu wa siku zake waliodhania kwa kutii kidogo sheria za Musa, watapata uzima wa milele, lakini wakasahau amri ya kwanza ambayo ni, "mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote." Basi watu wengi wanaamini wao ni wakristo na wamefunzu kwenda mbinguni, kwa sababu wanaenda kanisani na kuimba tenzi na kusema amina kwa maneno yaliyoandikwa, ambayo mhubiri anayasema, basi wengi hawa jafundishwa kile ambacho Mungu anataka, zaidi ya vyote ni ushirika wa ndani na watu wake, ambapo ndipo mahali mambo mengine yatachibukia.

Mathayo sura ya 7 msitari wa 21 hadi 23, kwa pamoja inaeleza maneno ya Yesu kuhusu siku ya hukumu ya mwisho wakati wengi watakuja kwake wakizungumzia matendo yao mema. "sio kila mtu anitaye Bwana Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; mbali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? .ndipo nitawaambia dhahili, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu."

Hakatai kuwa watu hawakufanya walichokiri, lakini anakataa kuwa hawakuwa na uhusiano wa sawa na Yeye. Wanaonekana kana kwamba walimjua lakini hawakumjua kama Bwana na mwokozi wao binafsi. Sio kupitia matendo mtu anapata kuokolewa ni kupitia imani pekee (ni uaminifu na uhusiano wa upendo) na Mungu.

Katika Yohana sura ya 4 msitari wa 21 hadi 24, kwa pamoja, Yesu anazungumza na mwanamke Msamaria ambaye alikuwa anamsubiri kisimani wakati wa jua kali wa mchana, mazungumzo yanaazishwa na Yesu akisema kitu ambacho kinahusika kwake, na kwa kasi mazungumzo yanazunguka mpaka kujizungumzia mwenyewe, na mwanamke anahitaji kumjua yeye.

"Yesu akamwambia, mama unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunakiabudu tukijuacho; Kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja na sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika Roho na kweli.

Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho nao wamwabuduo ina wapasa kumwabudu katika Roho na kweli." Mambo haya ni sawa nasi leo hakuna kiasi cha matendo mema kinaweza kutuokoa kama vile wokovu ni kwa neema kupitia imani na kumwamini Yesu Kristo.

Kuabudu kwa kweli kuna weza kutoka kwa mtu ambaye yuko katika uhusiano wa kweli na Mungu. Watu wengi leo wanaabudu vitu vingi tofauti, kwa wengine Mungu wao ni tumbo zao, basi wanaabudu kupitia kula vyakula tofauti. Kwa wengine Mungu wao ni mvinyo basi wanalewa kila wakati kwa bia au mvinyo. Kwa wengine ni mpira wa kandanda, na kwa wengine pia ni gari lao au kumiliki kustahili kukubwa, hata hivyo Yesu anataka kuwa yeye

pekee ndiye ambaye unamwabudu, haimanishi hautafurahia vitu hivi viingine pia, (kwa kiasi) lakini unapotumia muda mwingi kwa hivi kuliko ule unatumia mbele ya Mungu kwa kumwabudu, basi unamyima Yeye haki yake ya nafasi katika maisha yako.

Kulikuwako wakati mmoja na Mwijilisti aliyetembea ulimwenguni kote akifua nafsi kwa Kristo, katika wakati wa kuishi kwake. Kabla ya mkutano wa dhara alituma wafanyakizi wengine kufundisha, waliojitolea jinsi ya kuhudumia wengine waliokuja mbele ya mkutano wakati wa kile kinaitwa saa ya wokovu, jioni moja somo la ujumbe ambao mnenaji huyo alikuja kunena ni wa umuhimu na matokeo ya kusifu na kuabudu.

Akazungumza karibia saa moja unusu katika somo hili, akionyesha mifano mingi kutoka kwa maandiko ilikusaidia pointi zile alizotaka kutoa. Moja ya pointi yake ilikuwa kwamba tusimwabudu Mungu kama kazi tunayostahili kufanya kutoka kwa mioyo yetu, lakini kama tunaotamani kumwabudu, kwa sababu anastahili, kwa sababu tunampenda na kwa sababu sisi ni watoto wake na ni jambo la kawaida kufanya.

Alipomaliza alichotaka kusema kakika somo aliketi chini, na yule aliyemwalika akasimama afunge mkutano. Kabla hajasema kitu akaangalia saa yake na akaona mkutano umejukua muda mchache kuliko kawaida, ambapo alisema: "Basi inaonekana tuna dakika chache ilituweze kurudi katika sifa na kuabudu kwa muda mfupi."

Hakusema hili kwa sababu yeye na waliohudhulia walitaka kufanya hili, alifanya hili kutoka kwa hisia za wajibu kwa Mungu, akifikiria kuwa atakuwa anamwibia Mungu iwapo mkutano utaisha mapema. Hili lilikuwa swala ambalo mnenaji alitaja, kuwa tusimsifu na kumwabudu Mungu kwa sababu ni kitu cha kufanya au kujazilia muda mchache, kama sivyo mkutano utaisha mapema, lakini kwa sabanu haya ndio yaujazayo moyo wetu, na unatuambia tuyafanye.

Hakuna dhambi kuamaliza mkutano mapema iwapo ujumbe umemalizika mapema kuliko kawaida. Yote ni kulingana na hali ya ndani ya uhusiano mtu alionao na muumba wake. Hili ndilo linalo hesabika sana. Kwa huzuni kuna wengi wanaohudhulia mikutanoni juma kwa juma, na kupitia kama mwendo, hakuna kweli ndani ya mioyo yao kabisa, wanafuata tu kile ambacho wengine wanafanya.

Mungu anataka kusifu na kuabudu kwa mioyo yetu, anapopokea tutoke mkutanoni tukiwa tumetiwa nguvu kiroho, tumeinuliwa na kutiwa moyo na kujua kuwa tunabeba uwepo wa Mungu nasi popote tuendapo. Kwa hakika hii ndiyo maana ya kusifu na kuabudu.

back to main articles page