Mbinu za kuwa na maisha yenye maombi ya kuguza na yenye nguvu

Keys to an effective prayer life

Kila momoja angetaka kuwa na maisha yenye maombi ya nguvu na yenye mguzo, lakini kuna vitu katika somo hili ambavyo wakristo wengi hawajafundishwa. Maombi ni kuongea na Mungu, hakuna zaidi wala hakuna chini ya hilo. Hili linaweza kufanyika mahali popote na wakati wowote. Zaburi 100 ni moja ya Zaburi zilizofupi (iliyo na msitari 5 pekee) hata hivyo ina mengi ya kutuambia kuhusiana na somo hili. "Mfanyie Bwana shangwe, dunia yote. Mtumikieni Bwana furaha: Njooni mbele zake kwa kuimba.

"Ninajua kuwa Bwana ni mwema: ni yeye aliye tuumba, na sio sisi wenyewe; sisi ni watu wake, na kondoo wa malisha yake. Ingia malangoni mwake kwa sifa, na nyuani mwake kwa kushukuru, ribariki jina Lake. Kwa kuwa Bwana ni mwema; fadhili zake ni za milele; na kweli yake ya dumu katika vizazi."

Iwapo unataka Bwana asikie maombi yako na ayajibu, basi fanya kama vile hii zaburi inavyopendekeza, ingia malangoni mwake kwa sifa na nyuani mwake kwa kushukuru. Haimanishi kuwa hautashiliki naye moyo wako wakati ambao unapitia wakati wa shida, lakini kufanya hivi mwanzo inakusadia kupata mambo katika mtazamo wa sawa.

Tunastahili kuwa na shukrani sana, kwa kuokolewa na kuzimu, kupewa wokovu – hakikisho kuwa tutaishi milele mbele za Mungu mwenyewe, fadhili zake ni mpya kila asubuhi na upendo wake (kwako) unadumu milele na milele. Hiyo peke ni ya ajabu kutosha kumsifu Mungu kwa milele yote.

Unapokuwa na mtazamo wa sawa, basi unaweza leta mbele za Mungu chochote kilicho moyoni mwako, na inaweza kuwa atashiliki nawe yale yaliyo moyoni mwake pia. Zaburi 142 inatuambia kama ifuatavyo: "Kwa sauti yangu nalimlilia Bwana, kwa sauti yangu nitamwomba Bwana dua.

Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, shida yangu nitaitangaza mbele zake. Nilipozimia roho uliyajua mapito yangu; katika njia niendeyo wametitegea mitego. Utazame mkono wa kuume ukaone, kwa maana sina mtu anijuaye, makimbilio yamenipotea, hakuna wakunituza roho.

Bwana, nimekuita nikasema, ndiwe kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai. Usikilize kilio changu kwa maana nimedhihilika sana. Uniponye na hao wanaonifuatia, kwa maana wao ni hodari kuliko mimi. Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, kwakuwa wewe unanikirimu."

Wakati Daudi alikuwa anapitia wakati mgumu alimwaga shida yake mbele za Bwana, Na tunavyoona kutoka kwa Zaburi hii, aliondoka imani yake ikiwa imeongezeka kama sio kurejeshwa. Alianza kwa kumwambia Bwana shida yake na akaishia kuweka shida zake katika mtazamo wakati alikumbushwa jinsi Mungu wetu alivyo mkuu, na mwenye uwezo. Waziwazi tunaona kutoka kwa Zaburi hii Daudi alikuwa karibu sana na Bwana kupitia maisha yake ya maombi. Tunashiliki mambo haya na rafiki zetu wa karibu, na Mungu anataka sana tumchukue yeye kama rafiki wetu wa karibu kwa sababu hivyo ndivyo anataka kuwa kabisa.

Tunaweza kuongea na Mungu mahali popote na wakati wowote, hata hatustahili kuwa pekee yetu. Katika barua ya Paulo kwa kanisa la Efeso tunasona katika sura ya 5 mstari wa 18 na19: "Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi, na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshukuru Bwana mioyoni mwenu" Kwa njia nyingine wakati unapitia wakati wa shida usifanye kile ambacho watu wa ulimwengu wanafanya, na kujukua tabu zako kwa vinyuaji na kunywa mvinyo, lakini peleka shida yako kwa Bwana, na utapata kufaulu sana na kutosheka kwa kufanya hivyo. Watu wengi huzungumzia kuhusu wa Philipi sura ya 4 ms 19 kuwa ni utoaji wa Bwana lakini hawasemi chochote kuhusu 18.

Mistari hiyo miwili lazima ichukuliwe pamoja kama sivyo msitari ufuatao utakuwa nje ya mada. Msitari wa 18 na 19 inasema: "Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile viliotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impedezayo Mungu. Na Mungu wangu awajalizeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu." Misitari hii inasema katika matokeo kuwa iwapotuta wahudumia watu nje ya jamii zetu wenyewe na tuwe na ukarimu kwao basi na Mungu atatuangalia na awe mkarimu kwetu pia, hiyo ndiyo kanuni ya bibilia.

Mungu ana hamu sana ya kuwa tumuamini yeye na tuliamini neno lake, Basi ikiwa kuna shida katika maisha yetu au upungufu ambao unahitaji kushughulikiwa upesi leta mbele za Bwana, mwachie yeye na uamini kuwa atakupa hekima pia upambane na hiyo hali wewe mwenyewe au kuwa atapambana na hiyo hali yeye mwenyewe kwa niaba yako. Maombi ya shaka hayana uhakika wa kuzikilizwa. Wacha tuje mbele za Bwana kwa imani na kwa kushukuru.

Kuna mifano miwili kutoka kwa maandiko moja kutoka Agano la kale na mwingine kutoka kwa mfano Yesu alisema kuonyesha sisi kuwa kuna wakati maombi yetu yanastahili kuwa ya kuendelea pasipo kukoma, kabla hatujapata majibu yake ambayo tunatamani. Moja ni kwenye kifungu katika Danieli 10 mahali malaika anakuja kwa Danieli kumtia moyo.

Katika mistari ya 10 hadi 13 ya sura hii tunasoma: "Natazama mkono ukaniguza ukaniweka juu ya magoti yangu, na vitanga vya mikono yangu. Akaniambia, Ee Daniel, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, na lisimama nikitetemeka ndipo akaniambia usiogope Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipiga siku ishirini na moja; bali tazama huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko na wafalme Wauajemi."

Mfalme wa Uajemi sio mwanadamu lakini ni nguvu za mapepo, moja ya zile zinazo sababisha shida ulimwenguni. Hili halifai kututia hofu kwani tunaposoma katika Waefeso sura ya 6 msitari wa 12 na 13 inatukumbusha kuwa: "Hatufanyi vita juu ya damu na mwili, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya jeshi la pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kupiga na siku za uovu na mkiisha kuyatimiza yote kusimama." Mawaidha ya Agano jipya kuwa tunastahili kutokoma katika maombi yetu inakuja katika mfano Yesu alipeana unaojilikana kama mjane mng’ang’anifu, inapatikana katika Luka sura ya 18 msatari wa 1 hadi 8 inasema kama ifuatavyo:

"Akawaambia mfano, ya kwamba inawapasha kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaa. Akasema palikuwa na kadhi katika mji Fulani, hamchi Mungu wala hawajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea akisema, nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, lakini kwakuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake asije akanichosha kwa kunijia daima.

Bwana akasema, sikilizeni kama asemavyo yule kadhi mdhalimu. Na, Mungu je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?. Nawaambia, atawapatia katika upesi; walakini atakapo kuja mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?.

Ujumbe wa maandiko haya katika vifungu hivi viwili ni dhahiri, usikate tamaa kuombea kile unacho hitaji na kutamani kwa kuwa kuna vita vya rohoni vinavyoendelea katika ulimwengu

wa roho, isipokuwa kuna udhaifu kwako endelea kuomba na ujue kwelikuwa hatimaye utaona kile unachoomba kikitendeka.

Kunakitu kiingine kuhusu vita vya rohoni, ambacho Yesu aliwafundisha wanafunzi wake lakini kimesahauliwa, na kimepuuzwa sana na makanisa mengi ya leo. Mandiko haya yatakuja mara kwa mara katika somo hili kwa sababu yana umuhimu sana. Ya kwanza inapatikana katika injili ya Mathayo sura ya 13 msitari wa 29, na inasema ifuatavyo: "Amaawezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu?

Ndipo atakapoiteka nyumba yake." Ya pili inakaribia kufanana na hiyo inasema kama ifuatavyo: "Amini na waambieni, lolote mtakalolifunga dunuani litafungwa mbinguni: na lolote mtakalolifungua duniani litafunguliwa mbinguni. Tena nawaambieni wawili wenu wakikubaliana jambo na kuomba, watapewa na Baba yangu aliye mbinguni.

Mahali wawili wamekusanyika kwa ajili ya jina langu, nami nitakuwa katikati yao." Katika maandiko hayo yote hayo ndio Yesu aliwaambia wanafunzi wake. Iwapo hatutafanya vile ambavyo Yesu ametushauri basi hatutaona matunda yakitokea. Watu wengi wamekosa kuyafahamu au kufafanua kimakosa maandiko haya (katika hali zingine yote mawili) kama inavyosema wazi chochote utakachofunga duniani kitafungwa mbinguni na chochote unachofungua dunuani kitafunguliwa mbinguni. Usimwambie Mungu afanye kufunga na kufungua, hiyo ni kazi yako, Zaidi umepewa mamlaka kufanya, basi endelea na utumie hayo mamlaka Mungu amekupatia. Hakuna maana yako kuwa na mamlaka haya, iwapo Mungu atajifanyia mambo haya yeye mwenyewe.

Kunayo mambo katika mandiko ambayo tumeamriwa tuyaombee. Moja ya haya ni wale wote wanaotuongoza. Hiyo ina maanisha serikali ya mtaa na kitaifa, jeshi la polisi na chochote na kila kitu ambacho kina mamlaka ya halali juu yetu. Hapa hatuwahesabu wachungaji wetu na viongozi kama vile wamehesabiwa katika maandiko kama vile tunavyoenda kuona hivi punde.

1 Timotheo sura ya 2 msitari wa 1 hadi 4 ni muhimhu sana, sana katika somo hili tunaloliangalia, inasema: "Basi. Kabla ya mambo yote, nataka dua na sala, na maombezi, na shukurani, zifanyike kwa watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka tuishi katika maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri nalo lakubalika mbele za Mungu mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli."

Je, ni vipi kuhusu maombi kwa mtumishi wako, mchungaji na viongozi? Kuna msitari unaohusika na hilo lazima tuende katika kitabu cha Mwanzo sura ya 17 msitari wa 9 hadi 13 inayosema kama ifuatavyo: "Musa akamwaambia Yoshua tuchagulie watu, ukatoke ukapigane na Wamaleki; kesho nitasimaa juu yac kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu.

Basi Yoshua akafanya kama vile ambavyo Musa alikuwa amemwaambia, akapigana na Wamaleki na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu yakile kilima. Ikawa Musa alipouinua mkono wake Israeli walishida; na aliposhusha mkono wake Amaleki walishinda.

Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe wakaliweka chini yake akalikalia Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu, mikono yake ikadhibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Wamaleki na watu wake kwa ukali wa upanga."

Katika maandiko hayo viongozi wa Israeli wakapokea ushidi mkubwa viongozi waliposhikwa mkono kuendelea, Hakika basi iwapotuta mwombea mchungaji wetu na viongozi kila siku (hata kama ni kwa muda mfupi) basi wataona ushindi mkubwa kinyume na adui pia.

Hata hivyo kuna vitu vingine viwili ambavyo lazima vizingatiwe. Moja ya hivi linapatikana katika Zaburi 66 msitari wa 18 inasema: "Kama ni ngaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia" Nyingine ni andiko ambalo wengi wanafikiri linahusika na mfano

ulionyuma yake lakini yote yako katika kifungu kimoja cha maneno ya Yesu kwa wanafunzi wake.

Haya yanaweza kupatikana katika Marko sura ya 11 mstari wa 20 hadi 26. "Na asubuhi walipokuwa wanapita waliona ule mtini umenyauka kutoka shinani. Petro akakumbuka habari zake akamwambia,, Rabi tazama mtini ulioulaani umenyauka. Yesu akajibu akamwambia mwaminini Mungu.

Amini nawaambia yeyote atakaye uambia mlima huu ng’oka uingie baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila amini hayo ayasemayo yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo na waambia, yoyote mwombayo mkisali, aminini ya kuwa mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

Nanyi kila msimamapo na kusali wasameheni, mkiwa na jambo juu ya mtu; ili baba yenu aliye mbinguni awasamehe nanyi makosa yenu. Lakini ikiwa ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye juu mbinguni hatawasamehe makosa yenu." Unataka kujua vile maombezi yako yanaweza kuwa yanguvu?

Ukitazama maandiko yafuatayo yatakupa msada katika hilo. Mwanzo sura ya 18 msitari wa 16 hadi 33 inatuambia, hadithi ya maombezi ya Ibrahamu na Mungu akiombea mpwa wake na familia ya Lutu. Wakati tunawafanyia maombezi waliopotea inastahili kuwa kama tuna jambo la binafsi kuona wamepokea wokovu.

Inasema hivi: "Kisha watu hao wakatoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaondoka nao awasindikize. Bwana akanena, je, nimfiche Ibrahamu jambo nilifanyalo, ikiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari na katika yeye mataifa yote ya dunia yatabarikiwa?

Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake washike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake. Bwana akasema kwakuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana, basi nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilicho nijia na kama sivyo, nitajua.

Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana. Ibrahimu akakaribia akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Huenda pakawepo wenye haki hamsini katika mji, utahalibu wala hautauaja mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo?

Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu hasha; Mhukumu ulimwengu asitendete haki? Bwana akasema nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.

Ibrahimu akajibu akasem, basi nimeshika kunena na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu. Huenda wakapungua watano kwa hao hamsini wenye haki, je, utahalibu mji wote kwa kupungua kwa hao watano? Akasema sitauhalibu, nikiona humo arobaini na watano. Akazidi tena kusema naye akinena huenda, huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema sitafanya kwa ajili ya hao arobaini. Akasema Bwana asiwe na hasira nami nitasema, huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema sitafanya nikiona hao thelathini.

Akasema tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. Akasema Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, huenda wakaonekana huko kumi? Akasema sitaharibu kwa ajili ya hao kumi. Basi Bwana alipo maliza kusema na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimui naye akaenda mahali pake"

Mfano mwingine mkubwa unapatikana katika Danieli sura ya 9 wakati Danieli anawafanyia maombezi watu. Katika Danieli 9 msitari wa 15 hadi 21, tunapata taswira yayaliotokea wakati Danieli alikuwa mbele za Mungu akiwaomea watu wa Israeli. "Na sasa Ee Bwana Mungu wetu, uliye watoa watu wako hawa katika nchi ya Misri kwa mkono hodari, ukajipatia sifa kama ilivyo leo.

Tumefanya dhambi, tumefanya maovu. Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, milima wako mtakatifu, maana kwa sababu ya dhambi zetu na maovu ya baba zetu, Yerusalemu watu wako wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka.

Basi sasa Ee Mungu wetu, yazikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazie uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa kwa ajili ya Bwana. Ee Bwana Mungu wangu tega sikio lako usikie, fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako, maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi.

Ee Bwana usikie, Ee Bwana usamehe, Ee Bwana usikilize, ukatende, usikawie; kwa ajili yako wewe, Ee Mungu wangu; kwa sababu mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako. Basi hapo nilipokuwa nikisema na kuomba, na kuungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, nakuomba dua yangu mbele za Bwana, Mungu wangu, juu ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu; Naamu nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule Gabrieli niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, aliniguza panapo wakati wa dhabihu ya jioni." Je, nimatokeo gani yatatokea iwapo utaanza kuombea taifa lako kwa njia hii? Je, ni jambo ambalo unahesabu la maana kujaribu?

Mwisho maandiko yanazungumzia njia mbili za kufunga, tunastahili kufanya yote. Ya kwanza ni kile Yesu alifundisha wanafunzi wake wafanye. Na ya pili inatoka katikas kitabu cha Isaya. Katika Israeli na katika kitabu cha Matendo Yesu na wanafunzi wake wangefunga kwa sababu nyingi, ambazo zimewekwa wazi katika maandiko.

Mwelekeo, maombezi, hekima, maagizo kutoka kwa Mungu, utambuzi, uponyaji na ukombozi. Kama vile Yesu alivyofanya hivyo na kuwa wafundisha wanafunzi wake kufanya hivyo twafaa kufanya hivyo pia. Kufunga ni kuenda bila chakula kwa mfano masaa 24 na kunywa maji tu pasipo kufuatanisha.

Kuna kufunga kwingine ambako kunajulikana katika Isaya sura ya 58 msitari wa 6 hadi 8 inasema: "Je, saumu niliyoichagua siyo namna hii? Kuvifungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? Je, siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako?

Umwonapo mtu aliyeuchi umvike nguo wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe. Ndipo nuru yako itakapo bambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara, na haki yako itakutangulia, utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde."

Yakobo sura ya 1msitari wa 22 inasema kama ifuatavyo: "Lakini iweni watendaji wa neno, mbali sio wasikiaji mkijindanganya wenyewe." Kila mkristo anastahili kuwa mtendaji wa neno na sio msikiaji tu. Iwapo tutazonga mbele na kufanya mambo ambayo tunajifunza basi lazima ulimwengu utakuwa mahali tofauti. back to main articles page