Bwana wa mavuno

God of harvest Hadithi ya Yesu, ya kwanza kuwatuma wanafunzi wake pamoja na watu wengine 60, katika uwanja wa mavuno na nguvu za kukemea mapepo, kuponya wagonjwa na kuwafufua wafu, ni yenye kujulikana lakini kuna alama muhimu katika misitari ya kwanza michache ambayo imepuuzwa ingawa ni muhimu sana. Hebu tutazame kifungu chote kwanza kisha tuangalie alama muhimu zilioko ndani.

"Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. Akawaambia mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache, basi mwombeni Bwana wamavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.Enendeni, angalieni, nawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu. Msichukue mfuko wala mkoba, wala viatu, wala msimwamkie mtu njiani.

Nyumba yeyote mtakayoaingia kwanza semeni, amani ikuwemo nyumbani humu. Na akiwemo mwana waamani, amani yenu itamkalia, la hayumo amani yenu itarudi kwenu. Basi kaeni katika nyumba hiyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao, maana mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame ha me kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.

Na mji wowote mtakaouingia wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekavyo mbele yenu, waponye ni wagonjwa waliomo, waambieni ufalme wa Mungu umwekaribia. Na mji wowote mtakaouingia nao hawakaribishi tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni, hata mavumbi yalio katika mji wenu yaliogandamana na miguu yetu tunaya kung’uta juu yenu. Lakini jueni hili yakuwa ufalme wa Mungu umekaribia. Nawaambia yakwamba siku ile itakuwa rahisi sana Sodoma kustahimili adhabu zake kuliko mji huo.

Ole wako Korazini! ole wako Bethsida! Kwa kuwa kama miujizahiyo iliyofanyika kwenu ingelifanyika katika Tiro na Sidon, wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu. Lakini siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu yake kuliko niyni. Nawe Kapernaumu, utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.

Awazikilizaye ningi anizikiliza mimi naye anikaataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakasema, Bwana hata mapepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia, nalimwona shetani akianguka kutoka juu mbinguni kama umeme. Tazama, ni mwewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui wala hakuna kitu kitakacho wadhuru. Lakini msifurahi kwa vile mapepo wanavyowatii, bali mfurahi kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.

Tuaona Bwana aliwachagua watu 72, nasio 12 tu, kuenda sehemu ambazo yeye mwenyewe alikuwa anaelekea. Kwanini afanye hivi – ni kusudi gani 72 wako nalo kwenda katika sehemu hizi, sana sana kwenda katika vifungu? Vyema iwapo utawahi kupata nafasi ya kuombea watu ni wazo zuri kufanya kwa makundi, ilikwamba mtu anaweza kuzikiliza kile ambacho mtu anasema na mwingine anaweza kuzikiliza nini Bwana anasema.

Iwapo kuna mapepo yatajionyesha yatastahili kukemewa, kiroho kila wakati, lakini katika hali nyingine itahitaji kujizuia kimwili kwa mtu aliye na roho chafu ndani yake. Ingawaje mtu mmoja anatosha kukemea itoke hata pepo yenye nguvu, mtu anayefanya ukombozi anawezakuwa hana ufahamu, au kukosa imani au anasitasita mbele ya mapepo kwa udhaifu. Mtu ambaye anahudumu na wewe, anaweza kuwa na uwezo na kutumia ufahamu wake na aiokoe siku inavyokuwa.

Kanuni hiyo hiyo inatumika wakati unawaombea wagonjwa, mtu mmoja akiwa anamzikiliza mtu na mwingine anaweza kuzikiliza nini Mungu anataka kusema kwa neno la maarifa na/au kutiamoyo. Iwapo utamwuliza Bwana jinsi ya kuomba katika kila hali basi atafanya hivyo. Yesu aliwaponya wagonjwa na akakemea mapepo kwa neno basi kwanini tuhitaji kuchukua dakika kumi kuombea kila mtu binafsi?

Sababu ya Yesu kuwatuma wawili wawili ilikuwa, ni iliwafanye kile ambacho Danieli alifanya katika sura ya 9 ya kitabu hicho katika bibilia. Fanya uchunguzi ujue dhambi za sasa sa mahali hapo na zile dhambi za akina baba katika siku ziliopita. Kisha kiri mambo hayo

mbele za Mungu pamoja na dhambi zako mwenyewe, na ni nani ajuaye, unaweza pata kutembelewa na malaika pia.

Usiwahi sahau kuwa nafsi zinafuliwa mahali pamoja na pamoja pekee, katika ulimwengu wa rohoni kupitia maombi, kisha unaenda na kuhubiri neno lililonenwa, neno la sasa ambalo Mungu atakupatia katika kila tukio (iwapo utamwomba) na utafua nafsi ambazo ulizimiliki katika ulimwengu wa rohoni kupitia maombi. Hili halitafanyika kwa usiku mmoja, lakini litafanyika tu kupitia maombi, na kufunga kila mara kwa majuma mawili kabla na usiku wa kuamkia mkutano.

Utahitajika kufaa silaha zote za Mungu, kwa sababu unastahili kutambua kuwa haufanyi vita juu ya mwili na damu, lakini juu ya masultani na nguvu za giza za anga zinazoonekana kutawala kizazi hiki, lakini ni nani ajuye ni uovu kiasi gani ambao Mungu ameuzuia katika ulimwengu, kwa sababu ya watu wanaomba kwa uaminifu, kinyume na nguvu za giza, katika maombi ya kila siku, na katika mikutano ya kila mara.

Wakati Yesu aliwaelezea watu hadithi ya mpanzi, Mathayo sura ya 13 msitari wa 1 hadi 9, Yesu anaaelezea kuhusu mbegu ziingine zilizoanguka kwenye kando ya njia, na zikaliwa na ndege wa angani, hizi zinawakilisha adui na nguvu zake zote ambao isipokuwa mamepaki kutekwa nyara atafanya chochote awezavyo kuziiba mbegu za neno la Mungun kutoka msikioni mwa wale wanalolisikia.

"Siku ile Yesu akaondoka nyumbani, akaketi kando ya bahari. Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi na ule mkutano wote wakasimama pwani. Akawaambia mambo mengi kwa mfano, akisema, tazama, mpanzi aliondoka kwenda kupanda. Hata alipokuwa akipanda, mbengu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila, nyingine zikaanguka penye miamba pasipo kuwa na udongo kukosa kina.

Na jua lilipozuka zikaungua, na kwakuwa hazima mizizi zikanyauka. Nyingine zikaanguka kwenye miiba, ile miiba ikamea ikaizisonga, nyingine zikaanguka kwenye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini. Mwenye masikio na asikie."

Siku moja kundi la maombi likiwa limepangwa katika mkutano na Mwinjilisti anayejulikana wa kimataifa. Walikuwa waombe siku zote za mkutano kuendelea mpaka umalizike. Katika usiku wa mwisho waliamua wafanye jaribio. Katika usiku wa siku tano zilizopita wakati kiongozi wa kundi hilo alifunga mkutano wasimama na kuacha kuomba.

Kwenye usiku wa mwisho, wakati kulikuwa na nafasi kwa watu ambao wangependa kumpokea Yesu katika maisha yao, waliendelea kuomba wakati kiongozi wa mkutano alikuwa ametangaza mkutano umefungwa. Walivyo zidi kuomba ndivyo watu wasonga mbele kumpokea Yesu, mpaka dakika 27 kuto-ka wakati mkutano ulikuwa umetangazwa kwamba umemalizika. Hii labda ni bahati tu au dhihilisho la nguvu za maombi

Moja ya mambo muhimu ambayo watu wanastahili kujua leo ni kuwa, ni kwanini wanahitaji Yesu. Kwa wengi (au kwa wote) shule za Uingereza hawaruhusiwi kufundisha Yesu kama mwana wa kipekee wa Mungu, na kuwa ndio njia pekee ya wokovu, lakini watu wameruhusiwa kufundisha mambo haya katika mikutano ya hadhara au kwenye mafundisho ya bibilia. Mpango wa wokovu ni rahisi kuelewa na kuelezea lakini watu wengi hawajasikia wazi zaidi na ya kutosha.

Mathayo sura ya 7 msitari wa 21 hadi 23 inazungumzia watu wakija mbele za Yesu katika siku ya mwisho wakitarajia kuingia mbinguni. "Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwajina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitakapo waambia dhahiri, siku wajua ninyi kamwe, ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu."

Ukristio sio kama nyingine zijulikanazo kama dini, sio kuhusu kutimiza sheria zilizowekwa siku baada ya siku, si kuhusu kufanya matendo mema lakini ni kuhusu uhusiano wa ndani wa binafsi na muumba wako. Watu wengi ulimwenguni wanaamini kuwa iwapo watafanya

matendo mema mengi na wasiwe watu waovu basi wame hakikisiwa kuingia mbinguni. Watu hawa walifanya kazi lakini hawakuwa na uhusiano ambao ungewaokoa.

Watu wenyi pamoja na wahubiri wengine, ambao wamendanganyika wanaamini kuwa mbinguni na jehanamu zio halali, bali ni mambo ya kiakili, hata kama kuna kweli ambayo maandiko yameonyesha wazi kwamba mambo haya sio ya akilini bali ni kweli halisi. Iwapo utamwona mtu akiwa kwenye nyumba inayochomeka kwa moto na wanakiimbia mahali ambapo sio salama si utajkaribu kuwaita ilikuwaelekeza mahali salama iliwaepuke moto?

Watu wengi makanisani wanaamini kuwa uinjlisti ni kuhubiri injili wakati kuna wageni kanisani kwao. Ndio hili ni sawa lakini maandiko yanasema tunastahili kutoka nje kuhubiri injili kwa kila mtu. Ndio sababu uinjilisti unaitwa "kufikia" kwa sababu tunaenda nje ilikuwafikia wale ambao labda hawangeweza kuja makanisani kwetu kuisikia injili katika mahali pa kwanza.

Kuna mfano mzuri wa hii umeonyesha katika mfano wa sherehe ya arusi ya ambayo Yesu aliwaelezea watu na unapatikana katika Luka sura ya 14 msitari wa 15 hadi 24.Basi aliposikia hayo mmoja wale walioketi chakulani pamoja naye aliwaambia. "Heri yule atakaye kula mkate katika ufalme wa Mungu. Akawaambia mtu mmoja alifanya arusi akawaalika watu wengi,

Akamtuma mtumwa wake saa ya arusi awaambie wale walioalikwa, njoni kwa kuwa vitu vyote vime kwisha kuwekwa tayari. Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja, wa kwanza aliwaambia, ni menunua shamba, sharti niende nikalitazame, tafadhali unisamehe. Mwingie akasema, nimenunua ng’ombe njozi tano, nina kwenda kuwajaribu tafadhali unisamehe, Mwingine akasema nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.

Yule mtumwa akaenda akampa Bwana wake habari ya mambo hayo, basi yule mwenye nyumba akakasirika akamwambia mtumwa wake, "Toka upesi uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawale hapa maskini na vilema, na vipofu, na viwete." ‘Mtumwa akasema, Bwana hayo uliyosema yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi.’

"Bwana akamwambia mtumwa toka uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa. Maana nawaambia kweli hakuna katika walewalioalikwa hakuna yeyote atakaye ionja karamu hiyo." Mfano huu uliokuwa kabisa umeelekezewa wale ambao walikuwa wanatarajia kuwa arusini – katika arusi ya mwanakondoo mbinguni. Iwapo tumefanya kwa uaminifu kile ambacho Bwana wetu ametuamru na tutafute kumfuata siku baada ya siku basi tutakuwepo hapo, kwa hilo utakuwa na uhakika.

Lakini iwapo watu wamerundi nyuma wakateti na hawafanyi lolote kusaidia kuleta mavuno ya nafsi, hawajafanya lolote kusaidia maskini, hawajawahi kutembelea wagonjwa au wale waliotupwa gerezani basi kulingana na maandiko watu kasma hawa ndio watakaokosa kuwa kwenye arusi ya mwanakondoo mbinguni, ambayo kulingana na sherehe za Wayahudi kila wakati hufanyika kabla ya siku ya harusi. Iwapo hautachukuliwa wakati wa unyakuo basi utaishiliki kuzimu hapa duniani chini ya utawala wa mtu wa dhambi, shatani mwenyewe.

Ni nini unaweza kufanya hata kama Mungu hakuiti kwenda katika mataifa kama mwinjilisti? Orodha ni rahisi kuandika. Soma mafuzo ya bibilia ukitazama mambo haya katika maandiko ni njia moja, kumfunza mtu mwingine hiyo ni nyingine, njia ya tatu ni kufanya moja ya P, ingawaje utahitajika kufanya moja ya katika zile mbili za kwanza, unahitajika kujua P tatu zina simamia nini. P1 ni kuwaombea wale ambao wana mwito kwenda kuhubiri injili katika mataifa.

P2 ni kuwaombea watoke, au utoe kwa ajili ya matumizi yao au matumizi ya shirika ambalo lina watuma nje kwa jina la Yesu. P3 ni klutafuta uso wa Mungu uone iwapo anakuita wewe uwe mhubiri wa uinjilisti labda katika taifa hili au kimataifa. Pia kumbuka maneno ya Yesu Luka sura ya 10 msitari wa 1 hadi 3 unao nukuu Yesu akisema, "Mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache, basi omeni kwa Bwana iliawatume watenda kazi kwa mavuno yake."

Mwisho, katika mikutano mingi ya wainjilisti wagonjwa hupata kupona na hata pia miujiza miingine hufanyika kwa mfano kukemea mapepo, lakini nguvu hizi zatoka wapi? Matendo sura ya 1 msitari wa 8 unaonyesha wazi. "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu." Huu ni mstari ambao umeeleweka makosa basi tutajaribu kupata ukweli wake.

Luka sura ya 5 msitari wa 17 hadi 20: Ilikuwa siku moja Yesu akiwa anafundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Uyahudi, na Yerusalemu, na uweza wa kuponya ulikuwapo apate kuponya. Na tazama wakaja watu wamemchukua mtu kitandani mtu mwernye kupooza wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake.

Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa sababu ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha kwenye matofari ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katika mbele ya Yesu. Naye alipoiona imani yao, ailimwambia, "Ee, rafiki, umesamehewa dhambi zako." Kweli ambayo andiko hili linaonyesha, linaposema kuwa katika tukio hili nguvu za Mungu zilikuwa pamoja na Yesu ili kuponya, linapendekeza kuwa hili halikuwa kawaida.

Hili limezaliwa kutoka kwa maandiko mawili ya Agano Jipya, ya kwanza ni kutoka kwa Matendo sura ya 1 msitari wa 8 na ishaa nukuliwa tayari. Ya pili ni Yohana sura ya 5 msitari wa 19 inayosema: "Yesu akajibu akawaambia mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda, kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo mwana vile vile." Kwa njia nyingine inafanyika, "sio wakati nasikia kufanya lakini wakati namwona Baba akienda hiyo njia."

Yesu aliwaambia wanafunzi wake katika Marko sura ya 16 msitari wa 17 hadi 19 inayosema: "Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminiyo, kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya, washika nyoka hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu."

Mambo haya hayatafanyika wakati mtajisikia kufanya, lakini wakati wowote nitakaowambia kuyafanya mambo haya. Mamlaka yetu juu ya magonjwa, mapepo na kifo chenyewe ni yetu kupitia Kristo, ni nguvu zake zinazofanya kupitia sisi. Iwapo tutasonga mbele na kufanya kitu ambacho Mungu afanyi, basi tutapata kushindwa, lakini iwapo tutamgonja Mungu na tuache atuongoze tutaweza kupata ushidi, ni uzoefu na uhusiano wetu na Mungu pekee utatufundisha mambo haya, iwapo tuko tayari kujifunza.

Nguvu za Mungu zipo leo kuwaponya watu iwapo tu watu watafanya vile Yesu alivyofanya, na wasifanye chochote isipokuwa kile ambacho wanamwona Baba anafanya, kutakuwa na uponyaji mwingi na wakati mchache wa aibu za kushindwa ambao hakumtukuzi Mungu. Sawa sawa na uinjilisti, tunastahili kunena kile ambacho tunaambiwa kunena, na neno la Mungu litazaa matunda mengi na kufua nafsi nyingi kwa Bwana.

back to main articles page