Ukombozi

Deliverence

Iwapo nyumba yako itavunjwa, na iwapo kitu kimeibwa au la askari watafika, na kwa ajili ya manufaa yao na yako watakuwa wanatafuta ishara za ni vipi mwizi aliweza kuingia ndani. Iwapo hii ndio hali ya kimwili, kwa nini isiwe ndio hali ya rohoni? Kulikuwa na hadithi ya kupendeza sana ambayo inaoyesha umuhimu wa hili.

Kabla hajakuja katika taifa hili na kumtambua Bwana Yesu kama mwokozi wake, alikuwa amekua katika nchi ya kusini mwa nyaja, na familia ilikuwa inaabudu mungu wa kigeni. Wakati alikuwa na mazungumzo ya ajabu na ya miujiza kuhusu ukristo, alianza kwenda kanisa la nyumbani.

Walimpokea kwa mikono wazi lakini baada ya wakati mfupi, mapepo yalianza kujidhihirisha ndani yake wakati wa mikutano, ingawa kila wakati yalikemewa, yalionekana ni kama yalikuwa yakirudi. Basi suruhisho halikuwa sasa kuyatoa, kwa kuwa hilo lilikuwa rahisi, suruhisho lilikuwa ni kutafuta ni vipi yalikuwa yanaingia ndani, na ni vipi huo mlango wakuingilia waweza kufungwa kabisa.

Mchungaji na mdogo wake walikuwa na uzoefu wakutosha katika huduma, na hawa kuwa wanaelewa nini kilikuwa kinaendelea kufanyika, ni vipi mapepo haya yalikuwa yanaweza kurudi tena. Kisha pasipo kujua mgeni aliyekuwa amearikwa kuhubiri katika mikutano ya asubuhi, jumapili iliyofuatia alitambua mwanamke huyu alipagawa alipomwombea.

Akitambua kuwa ametoka Asia kusini alipanga kuwa naye pamoja na mshirika wa kundi lake, (pamoja na mme wake iwapo angependa kujiunga nao) kwa wakati wa huduma ya ndani. Ingawaje kwanza ukombozi haufanyiki, (hilo huja baadaye) anaulizwa kuhusu mavazi pamoja na vyombo ambavyo hupokea mara kwa mara kutoka kwa mamake, kutoka nje ya nchi na kwelezea vyombo alivyo navyo ndani ya nyumba yake na kabatini.

Inagunduliwa kuwa wakati wote kifurusi kidogo cha nguo kitamjia, ambacho huwa ni vazi la kitamanduni la nchi hiyo na itikandi. Tena inapatikana kuwa ana sanamu ya Buddha katika moja ya rafu zake, lakini sio sababu anapendezwa na mambo ya kiroho ya Buddha lakini kwa sababu ya mapambo yake.

Wachungaji wakaenda nyumbani na mme na mke, wakapita ndani ya nyumba wakiitakasa, na kutupa nje mavazi kutoka kabatini ambayo yana dhaniwa kuwa kuna uwezekano ndiyo yana sababisha shida yake. Kisha wanatupa nje vitabu ambavyo yeye na mme wake walikuwa wame kusanya kwa wakati mwingi, ambavyo vina masamo tofauti – yote yanahusiana na masomo ya uchawi.

Kisha wanatupa nje sanamu ya Buddha (hata igawea ni ndogo) pamoja na vitabu. Wanaweka vitabu kwenye chombo cha kuzolea taka cha chuma na kuvitia moto. Jambo ambalo sio la kawaida vitabu vile vinaruka kutoka motoni kisha vinarudishwa tena. Baada ya haya mwanamke huyo hakuweza kupagawa tena, na akakua kwa ajabu katika maarifa na ukomavu ndani ya Kristo na vipawa vya Roho Mtakatifu.

Wengine watapata mambo haya yakiwa magumu kuyaamini, lakini yale ambayo yametajwa katika somo hili ni yale ambayo yametajwa katika masomo mengine, hakuna nadhalia bali kweli iliyowazi. Kweli ni kuwa mavazi aliyokuwa anatumia yalikuwa yana laaniwa kabla kutumwa, na punde sanamu ya Buddha ilivyotupwa nje ya nyumba iliweza kupata anga tofauti kabisa.

Hii ndiyo iliyokuwa njia isiyo ya kawaida ambayo mapepo walipata kungilia ndani, sasa siri ilitambulika milango hiyo ilifungwa, na hakuna shida tena iliyoonekana. Kuna njia nyingi ambazo mapepo wanaweza kupata ilikuweza kuingia ndani ya watu, na kuwa sababisha kufanya yale ambayo wanajua kuwa hawastahili kuyafanya.

Orodha ifuatayo haija kamilika lakini ina njia chache ambazo hili laweza kufanyika: Tarot/kutabiri kupitia kandi (kupeana au kupokea), kusoma nyota, yoga, matibu kupitia kundungwa shidano, free mason, kutazama/kuzikiliza mazungumzo mabovu au nakala kama hizo, vingine vinajilikana kama vitabu vichafu, mizaa isiyofaa, mikanda chafu au michezo,n.k, sanaa za kijeshi, uganga (kupeana au kupokea), utambuzi kupitia maji au chuma (utambuzi wala sio uvumbuzi), usizi katika wakati wowote maishani, na wa aina yeyote, ulevi.

Kutosamehe (kuwa na kinyongo na mtu baada ya miaka mingi), ufutaji wa sigara, kuita roho za wafu, au kuwasiliana nao kwa njia yeyote, kuhusika kwa kuabudu miungu au kuwaheshimu, ujawi wa aina na mfano wowote, harufu ya tiba, maswali ya kuchanganya, uponyaji (ambao sio wa matibabu au wa aina sizizo kubalika na ukristo) ahadi ambazo hazija timizwa/makubaliano, kutenga kiumri, kutafakari mambo yanayojulikana, sanamu za miungu (haijalizi kama ni ndogo).

Kwa mfano sanamu ya Buddha, vitabu, magazeti, rekondi na mikanda inayo husiana na vitu hivyo viliotajwa yafaa kuharibiwa. Mziki wa sauti nzito, mziki wa rock, voo doo, na mizimu lazima pia ya jumlishwe kwenye orodha hii. Mapambo na mavazi yaliyonunuliwa au tengenezewa katika nchi za Bara ya asia yanaweza kuwa na laana kwa urahisi, iwapo una shuku yatupe.

Michezo ya video na talakilishi iliyo na ishara za mapepo, utambuzi, kuhusiana na wachawi, haijalishi ni waupe au sio, uchawi wa aina yeyote, wivu, tamaa, kiburi, husuda, uchungu. Iwapo ni wewe mwenye we au, ni mababu wako, au wazazi wako, au yeyote katika familia yako, amehusika katika aina yeyote ya mambo haya, yana stahili kukiriwa na kutubu, Kisha umulize Mungu akate kuunganika kokote na watu hawa juu ya maisha yako, na kuwasamehe watu dhambi hiyo.

Kwa sehemu kubwa, karibu kila tukio mtu hawezi kombolewa kutoka kwa pepo isipokuwa wame kubali. Jambo pekee lililo linyume na hilo limeandikwa katika Matendo sura ya 16 msitari wa 16 hadi 21 inayosema kama ifuatavyo: "Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliye kuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliye wapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwa hubiria njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi.

Lakini Paulo akisikitika akageuka akamwambia yule pepo, na kuamuru kwa jina la Yesu Kristo mtoke huyu, akamtoka saa ile ile. Basi bwana zake walipoona tumaini la faida yao limewapotea wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji. Wakawa chukuwa kwa makadhi wakasema, watu hawa wanachafua sana mji wetu, nao ni Wayahudi, tena wanatangaza habari ya desturi sizizo kuwa halali kwetu kuzisikia wala kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi."

Watu wengine wanaweza wakauliza ni kwa nini hii likawa hivi. Kwa njia ya mfano hebu tufikirie, kuwa una miliki nyumba, na uamue kumweka ndani mpangaji. Inawezageuka ikawa mpangaji huyo ni mtu mbaya na unaaweza kuchukizwa ni kwa nini ulimwingiza ndani, lakini kisheria hakuna kinachoweza kufanyika isipokuwa kumwamuru mpangaji huyo kuondoka.

Iwapo hataondoka kwa ombi la kwanza, basi mpangaji huyo anaweza ondolewa na askari kwa nguvu, kwa sababu basipo ruhusa yako, kisheria mpangaji huyo hana haki kukaa hapo. Mambo mengi yanafanana katika ulimwengu wa kiroho; hii ndiyo hali nyingine ambayo inafanana katika asili na kiroho.

Iwapo kweli uko ndani ya Kristo kabisa wewe ni mkristo moyoni mwako, na unaishi maisha ambayo yanaonyesha hilo, basi kwa sababu ya hili una haki ya kutoa amri ya kutoka, wakati una ruhusa ya mtu, na mtu huyo ni mkristo basi unaweza ,na kwa ujasiri kuamuru roho hiyo kutoka mara moja.

Iwapohauna uhakika wa mamlaka yako ndani ya Yesu kufanya hili, roho hiyo inaweza kushidana nawe, lakini iwapo una uhakika katika mamlaka yako kwa sababu ya nafasi yako ndani ya Yesu Kristo, basi una uhakika wa kufaulu.

Usikubali kuwa na mazungumzo na pepo mchafu, hilo ni jambo hatari kufanya. Yesu alilifanya mara moja tu wakati alikomboa pepo wa region kutoka kwa mtu, baada ya kuvuka mto. Hili lilikuwa kwa faida yetu ilikutuonyesha kuwa hata kama mapepo wengi wako ndani ya mtu, yana weza kuondolewa yote mara moja, kwa jina la Yesu – angalia Marko 5 kwa hadithi yote).

Katika Luka sura ya 10 wale 72 wanarudi kwa furaha, kuwa hata mapepo yanawatii, wakati wameyaamuru yamtoke mtu, lakini kumbuka mamlaka haya yanapatikana ndani ya jina la Yesu pekee, haya patikani kila unapojisikia, ni wakati tu Mungu amekuambia ufanye jambo hilo.

Iwapo mtu sio mkristo na hataki kumpokea Ysu kama Bwana na mwokozi, baada ya kukombolewa basi usijaribu kumkomboa, kwa faida yake. Yesu alielezea nini hufanyika kwa pepo mchafu wakati anapomtoka mtu. Hili linapatikana katika Luka 11 msitari wa 24 hadi 26.

"Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipoona husema, nitarudi nyumba yangu niliyotoka. Hata afikapo, akiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye wenyewe, wakaingia kukaa humo, na mtu yule hali yake ya mwisho ikawa mbaya kuliko kwanza."

Iwapo hujakuwa mkristo aliyejitolea, na wewe hauko imara na hauna moto kwa ajili ya Mungu, basi usijaribu kumkomboa mtu, Matendo sura ya 19 msitari wa 13 hadi 16 tunasoma: "Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagaliwa na pepo wachafu, wakisema, nawaapisha kwa Yesu yule anaye hubiriwa na Paulo.

Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu akawaambia, Yesu namjua na Paulo na mfahamu, lakini nyinyi ni nani? Yule mtu aliye pagawa na pepo akawarukia wawili, akawaweza, akawashida, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa."

Sababu ya kwanza iliyopelekea hili kufanyika ni kuwa hawakuwa waumini kamili, ndani ya Yesu wa injili, na pili hawa kuwa na mamlaka kufanya hili, kama vile Yesu hakuwa amewambia kufanya hili. Iwapo angekuwa amefanya hivyo roho hiyo haingeweza kuwadhuru.

Yesu alionyesha umuhimu wa maombi pamoja na kufunga, baada ya kugeuzwa, machoni pa wanafunzi wake wawili juu mlimani. Hadithi hii imenakiliwa katika Marko sura ya 9 msitari wa 14 hadi 29 inasema kama ifuatavyo: "Hata walipowafikia wanafunzi waliona mkutano mkuu wakiwazunguka, na waandishi wakijadiliana nao, Mara mkutano wote walipomwona walishangaa, wakamwendea mbio, wakamsalimu. Akawauliza, mnajadiliana nini nao? Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu, na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda, nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo wasiweze.

Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni kwangu. Wakamleta kwake hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa, naye akaanguka chini akagaa-gaa, akitokwa na povu.

Akamwuliza babaye, amepatwa na haya tangu lini? Akasema, tangu utoto, na mara nyingi amamtupa katika moto, na katika maji, amwangamize, lakini ukiweza neno lolote utuhurumie, na kutusaidia.

Yesu akamwambia, Ukiweza! yote yanawezekana kwake aminiye, Mara babaye yule kijana akapaza sauti akasema, naamini, nisaidie kutoamini kwangu. Naye Yesu akiona mkutano unakusanyika, mbio akamkemea yule pepo mchafu akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi na kuamuru umtoke huyu wala usimwingie tena.

Akalia akamtia kifafa akamtoka, naye akawa kama amekufa. Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama. Hata alipoingia nyumbani wanafunzi wake kwa faragha, mbona sisi hatukuweza kumtoa? Akawaambia, namna hii haiwezi kutoka kwa neno lolote isipokuwa kuomba na kufunga."

Cha kushangaza kutoka wakati wa Yesu tunaona kitu ambacho kinafanyika wazi wazi katika siku hii. Marko sura ya 1 msitari wa 23 hadi 28 inanakili nini kilichofanyika katika tukio moja, wakati Yesu akwenda hekaluni, siku ya sabato. "Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu, akapaza sauti akisema, tuna nini nawe Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Nakutambua unani, Mtakatifu wa Mungu.

Yesu akamkemea akisema, fumba kinywa umtoke. Yule pepo mchafu akamti kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka. Wakashangaa wote hata wakasema, Nini hii? Ni elimu mpya!

Maana kwa uweza awaamuru hata opepo wachafu, nao wamtii! Habari zi kaenea mara kotekote katika nchi zote kandokando ya Galilaya." Tunaona kutokana na hili pepo wanaweza kufikiria, kunena na kusikia, lakini tunaona kitu kingine katika Marko sura ya tano wakati Yesu alikemea mapepo wa Legioni kutoka kwa Wagerasi.

Hili linapatikana katika msitari wa 1 hadi 13. "Wakafika ng’ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi, na alipokwisha kushuka kutoka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu, makao yake yalikuwa pale makaburini, wala hakuna mtu yeyote aliyeweza kumfunga tena hata kwa minyororo, kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja vunja zile pingu, wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kushida, siku zote usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akapiga kelele na kujikatakata kwa mawe.

Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio akamsujudia, akapiga kelele kwa sauti kuu, akisema, nina nini nawe Yesu, mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. Kwa sababu amemwambia, ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. Akamwuliza jina lako nani? Akamjibu jina langu ni Legion, kwakuwa tu wengi.

Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile.Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha. Pepo wote wakamsihi wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe, nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili, wakafa baharini."

Kweli kuwa walimwuliza Yesu asiwatoe katika nchi hiyo, inamaanisha kuwa walikuwa, wafalme wa anga. Tunaona kumbukumbu ya aina hii katika Danieli sura ya 10 na Luka sura ya 4. Kwanza tutaangalia kumbukumbu la kitabu cha Danieli sura ya 10 msitari wa 4 hadi 14, inasema: "Na siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza, nilipokuwa kando ya ule mto mkubwa, Hidekeli; naliinua macho yangu, nikatazama, na kumbe mtu aliyevikwa nguo za kitani, viungo vyake vimefungwa dhahabu safi ya ufazi; mwili wake pia ulikuwa kama zabarajadi safi, na uso wake mfano wa umeme, na macho yake kama taa za moto, na mikono yake na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu.

Nami Danieli nikaona maono haya pekee yangu, maana wale watu walikuwa pamoja nami, hawakuyaona maona haya; lakini tetemeko kuu liliwashika, hata wakakimbia kujificha, basi nikaachwa mimi peke yangu nikaona maono haya makubwa, wala hazikubaki nguvu ndani yangu; maana uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikuzasiwa nguvu.

Walakini naliisikia sauti ya maneno yake, ndipo nikashikwa na usingizi mzito, na uso wangu umeielekea nchi. Natazama mkono ukanigusa, ukaniweka juu ya magoti yangu, na vitanga vya mikono yangu. Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, fahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka.

Ndipo akaniambia, usiogope, Daniel; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi, alinipiga siku ishirini na moja; bali tazama huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi."

Mfalme wa Uajemi sio mwanandamu, lakini ni ni nguvu za pepo mchafu anayetawala juu ya eneo la Uajemi. Tunaona kutoka Luka sura ya 4 msitari wa 5 hada 8, ya kuwa moja ya majaribu ambayo Yesu alikumbana nayo, ni kupewa mamlaka ya kutawala ulimwengu iwapo angeinama na kumwabudu shetani.

"Akampandisha juu akamwonyesha milki zote za ulimwengu, kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia nitakupa wewe enzi hii yiote, na fahali yake, kwa kuwa imo mkononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia, imeandikwa, msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake."

Ibilisi alipata vipi mamlaka haya ya kutawala falme zote za ulimwengu? Jibu ni kuwa katika Mwanzo sura ya 1 msitari wa 28 tunasoma kuwa Mungu alimpa Adamu na Hawa mamlaka kutawala ulimwengu wote kwa niaba ya Mungu. Mungu akawa barikia, Mungu akawambia, zaeni mkaongezeke, mkaiojaze nchi na kitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."

Wakati Adamu alitenda dhambi katika bustani mwa Edeni kwa kumwasi Mungu, walipoteza haya mamlaka kwa ibilisi. Katika majaribu yake jangwani Yesu aliyashinda yakarudi kwa mwanadamu. Tunaona kutoka Luka sura ya 4 msitari wa 5 hadi 8 tunasoma: "Akampandisha juu akamwoyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia nitakupa wewe enzi hii yote na fahali yake, kwea kuwa imo mkononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo.

Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia, imeandikwa, msujudie Bwana Mungu wako yeye peke yake." Kwa sababu Yesu aliyashinda majaribu yote ya ibilisi aliwashidia wanandamu wote mamlaka makuu na kuwarudishia tena, laskini iwapo tu mamlaka hayo yanatumika inavyostahili, katika jina lake.

Pepo ni malaika aliyeasi na kuungana na ibilisi kwa jaribio la kumtoa Mungu mamlakani. Jaribio hilo halikufaulu lakini thuluthi tatu ya malaika wamendanyanywa. Ngao yetu kwa maovu yote wanayojaribu kuleta maishani mwetu ni ni kama ifuatavyo: silaha zote za Mungu, maombi, neno la Mungu na nguvu zake.

Katika Mathayo sura ya 28 msitari wa 18 hadi 20, Yesu alinena baadhi ya maneno yake ya mwisho kwa wanafunzi wake, baada ya ufufuo wake. Aliwambia: "Yesu akaja kwao, akasema nao, akawambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi; natazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Amina." Basi sasa hebu twendeni kwa ujasiri na kutumia mamlaka tulionayo katika jina la Yesu.

back to main articles page