Kujenga uhusiano utakao dumu milele.

Building a relationship that will last forever

Katika mataifa mengi ya magharibi, wakati mke na mume wanataka kuchukua mtoto asiyekuwa wao, wa wazazi wengine kisheria, wamtunze hata kama inaweza kuwa w ana mtoto wao, watatembelea makao ya watoto baada ya kuhojiwa na waakirishi wa makao ya watoto ilikuona iwapo makao yao yako salama kumchukua mtoto mwingine, wamlishe na hata kutimiza mahitaji yake mengine kwa njia yote wakati mtoto ni mgonjwa na watamtia moyo motto akue katika ya hatua inayohitajika kufikia uwezo wake Iwapo mambo haya yakuwa sawa, wazazi wanaotaka motto watapelekwa katika sehemu ya jingo mahali kuna watoto wengi wanao hitaji kuchukuliwa, waongea na kila mtoto mmoja mmoja kisha watapata yule ambaye kuna kushikamana kwa asili kati ya wazazi na mtoto.

Wakati hili litafanyika wazazi watamtembelea mtoto huyo kila wakati, ili mtoto huyo aweze kuwajua na wao watapata kumjua mtoto zaidi na zaidi. Iwapo yote yataenda sawa, basi mtoto atakuwa tayari na furaha kuondoka mazingara yake ya sasa, na apate kuishi ndani ya familia ya wazazi ambao kisheria watakuwa kama wazazi wa mtoto ua wasimamizi.

Hii imekalibiana na kile ambacho kinafanyika kati ya Mungu na mwanadamu. Hata ingawa Mungu anatujua sawa, na alijua yote kutuhusu hata kabla hatujazaliwa, hukumjua yeye mpaka ulipojibu kumsongelea kwa Roho Mtakatifu.Yeremia sura ya 1 mstari watano unasema: "Kabla sijakuumba ndani ya tumbo nilikujua; na kabla hujatoka ndani ya tumbo nilikutakasa, na nikakuweka uwe nabii kwa mataifa".

Ingawaje hatuna mwito sawa na huo, inatuambia kuwa Mungu alijua na akatupenda sisi hata kabla hatujaumbika, na akaweka kusudi letu ndani yake litakuwa nini. Kujenga uhusiano na Mungu ni sawa navile unvyojenga uhusiano na mtu mwingine; unaanza kuwajua, unakaa na wao muda mwingi zaidi na zaidi baadaye unaanza kuwapenda, na kihalali una shikamanishwa na wao kwa umilele.

Uhusiano kama ule Yesu alikuwa nao na Babake hauna tofauti, na jinsi ya uhusiano wa ndani ambao Mungu anatamani awe nao na kila mmoja wetu. Katika misitari saba ya kwanza ya Waefeso sura ya 1, tunasoma kitu ambacho hakijawekwa wazi na waalimu, lakini ni cha muhimu sana. "Paulo mtume wa Yesu kristo kwa mapenzi ya Mungu, kwa wateule walioko Efeso. Na kwa waaminifu katika Kristo Yesu: neema na iwe kwenu, na amani, kutoka kwa Mungu baba yetu, na Bwana Yesu Kristo.

Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo: kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla kuwekwa misingi ya ulimwengu, ilituwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo, kwa kuwa alituchagua, ilitufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na Uradhi wa mapenzi yake, na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo mpendwa. Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake." Mistari hiyo inaendelea na sura yote ya kwanza ya Waefeso kwa hakika mwanzoni iliandikwa kama sentezi moja.

Jambo muhimu ambalo halizungumziwi na waalimu na wahubiri ni kuwa mambo yalikuwa tofauti katika siku za Paulo, na hata kama ni tofauti sasa Paulo alichagua maneno yake kwa uangalifu sana, iliyaonyeshe alichomaanisha. Katika siku hizo iwapo mwanao mzaliwa wako ameasi kinyume nawe, kulikuwa na sehemu kwako ambayo ina kuruhusu wewe kumtenga na urithi wa mali yako, kumtenga kabisa na kutangaza hadharani.

Hakuna sheria kama hiyo kwa wale waliochukuliwa na wazazi wasio wazaa ilikuwalea; hawangetolewa katika maandishi ya urithi wa baba aliye wachukuwa kuwalea au kutengwa hadharani au faraghani. Hii ina kuonyesha kilindi cha ulinzi wetu katika Kristo, Aliahidi hatatuacha wala kutukana na hapa tuna uhakikisho zaidi.

Kuelekea mwisho wa kitabu cha Waefeso katika sura ya 5 msitari wa 18 hadi 21 Paulo anaandika kitu ambacho kinatupatia siri ya vile ambavyo tunaweza kujenga uhusiano wetu na baba wetu wa mbinguni wa ndani kama ule ambao Yesu alikuwa nao na Mungu alipokuwa anaishi kwa mwili wa mwanandamu alipokuwa hapa duniani, akijipeana mwenyewe kwa upungufu wote ambao tuko nao.

Mstari ulio katika swali unasema: "Msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni huku, mkiimba na kushangilia Bwana, mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana Yesu Kristo; hali mnajinyenyekesha katika kicho chake Kristo." Ni kicho gani hicho cha Kristo? Vyema hilo ni somo lingine kwa pamoja.

Iwapo tutafuata ushauri wa Paulo na kuimba nyimbo za rohoni kwa Bwana, basi tunakiingiza ndani kitu ambacho kimesahaurika na makanisa mengi kwa karne nyingi, na hicho ni kipawa cha maombi ya kimya. Hii inamaanisha unaweza kuwa unaomba, ukisifu na ukimwabudu Mungu ndani ya roho yako na umati wa watu wakiwa wamekuzunguka, na hakuna yeyote isipokuwa wewe na Mungu mtajua hili linaendelea.

Kuna mfano wa maombi ya kimya kitambo kama mwanzo sura ya 24 na msitari wa 45, hata ikiwa tafsiri zingine zina kosa maana ya msitari huu kwa pamoja. Kimo cha hadithi hii kinaweza kupatikana katika misitari ya 37 hadi 48 pamoja ya sura hiyo.

Msitari unasema ifuatavyo: Kisha bwana wangu akaniapisha akisema usimtwalie mwanangu mke wa binti za Wakanani, ambao nakaa katikati yao: ila uende mpaka nyumbani kwa baba yangu, na kwa jamaa zangu, ukamtwalie mwanangu mke. Nikamwambia bwana wangu, labda huyo mwanamke hatafuatana nami?

Akaniambia, Bwana, ambaye naenda machoni pake, atapeleka malaika wake pamoja nawe, atafanikisha njia yako; nawe utamtwalia mwanangu mke katika jamaa zangu, na wa nyumba ya babangu: ndipo utafunguliwa kiapo changu hapo utakapowafikilia jamaa zangu; nao wasipokupa msichana huyo, utafunguliwa kiapo changu.

Nami nikanja leo kisimani nikasema, "Ee Bwana, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, ukinifanikisha sasa njia yangu niendayo mimi; tazama! Nime simama karibu na kisima cha maji, basi naiwe hivi, msichana ajaye kuteka maji nikamwambia, Nipe, nakuomba, maji kidogo katika mtungi wako ninywe,: naye akaniambia, unywe wewe, na ngamia zako pia nitawatekea, huyo na awe ndiye mke BWANA aliyemwekea mwana wa bwana wangu.

Hata kabla sijaisha kusema moyoni mwangu, tazama, Rebeka akatokea na mtungi begani mwake; akashuka kisimani akateka. Nami nikamwambia, Tafadhali nipe maji ninywe. Akafanya haraka akatua mtungi wake chini, akanena, unywe na ngamia wako nitawanywesha pia.

Kisha ni kamwuliza nikasema, Ubinti wa nani wewe? Naye akasema, mimi ni binti Bethueli, mwana wa Nahori, Milka aliyemzalia. Nami nikamtia hazama puani mwake na vikuku mikononi mwake: Nikainama, nikamsujudia Bwana, nikamtukuza Bwana Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, aliyeniongoza njiani, nimtwalie mwana wa bwana wangu binti wa ndugu yake."

Ni nini "maombi ndani ya moyo wangu"? Bila shaka haya ni maombi ya kimya. Yesu anaonekana kuyatumia wakati mwingi katika uhusiano na Baba yake alipokuwa nje na ndani ya miji aliyoitembelea. Tunaona katika Marko 10 mstari wa 46 hadi 52 pamoja kwamba hapa inaonyesha kuwa ni hivyo: Wakafika Yeriko; hata alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo Yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia.

Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupasa sauti yake, na kusema "Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu. Na wengi wakamkemea ilianyamaze lakini alizidi kupasa sauti, Mwana wa Daudi unirehemu. Yesu akasimama akasema, mwiteni. Wakamwambia jipe moyo anakuita.

Akatupa vazi lake akaruka, akamwendea Yesu. Yesu akamjibu, akamwambia, wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akasema mwalimu wangu natakta nipate kuona. Naye Yesu akamwambia, Enendazako imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani." Iwapoutaona mtu amebeba koti ambalo linavaliwa na vipofu pekee na amebeba fimbo nyeupe mkononi mwake akikuita, je, utafikiria sababu yake ni nini?

Hapa Yesu inaonekana ametulia kidogo alipomwuliza mtu huyu kipofu alikuwa anataka Yesu amfanyie nini. Yesu hakuhitaji kuambiwa, ilikuwa ni karibu na chochote cha kawaida kinachoweza kufikiwa, na haikuwa kusikia imani ya mtu huyo pia. Iwapo utaangalia katika maandiko utapata kwamba Yesu aliwaponya watu vipofu katika njia tatu tofauti.

Kile ambacho kinaonekana kingeweza kufanyika hapa ni kwamba mtu huyu alipokuwa anamwendea Yesu, alimwuliza Baba atafanya nini katika jambo hili. Yesu angefanya chochote bila maagizo kutoka kwa Baba yake tunapoona baadaye, lakini kwa sababu ya uhusiano wake na Baba yake, Yesu alikuwa na uwezo wa kupokea maagizo kutoka kwake wakati wowote.

Huu ndio mfano wa uhusiano wa ndani ambao Mungu anatamani kuwa nao nasi, mahali ambapo tunasakia sauti yake na hapo tunatii maagizo yake kwetu. Hakukuwa na vikwazo vingi wakati wa Yesu kama ilivyo siku za leo; hili lote ni jambo la kibao mbele. Kwa sababu Yesu wakati wote alitembea katika ushirika na Babake, alikuwa na uwezo wa kusikia kutoka kwake wakati wowote, na alipotenda kwa utiifu kwa maagizo ya Baba yake Yesu alijua atafaulu kama vile usiku unafuta mchana.

Tunastahili tuwe kama Yesu katika heshima zote, lakini sana sana katika heshima hii. Katika Yohana sura ya 5 msitari wa 19 Yesu anawambia wanafunzi weke: "Yesu akajibu akawaambia mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile amwona Baba analitenda kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo mwana vile vile." Kama Yesu hangeweza kufanya chochote isipokuwa mambo yale ambayo alimwona Baba yake akifanya tujiuliza ni muhimu jinzi gani kwetu kuwa na uhusiano wa ndani na Mungu kwa ajili yetu wenyewe leo hii.

Labda unashangaa sauti ya Mungu inafanana na sauti gani, na vipi unaweza kutambua sauti 3 za Bwana kutoka kwa sauti zozote unazoweza kusikia. Katika maandiko kuna kama mara 4 wakati mmoja yanajaribu kuonyesha sauti ya Bwana iko vipi, wakati wa kwanza katika kutoka sura ya 20 mstari wa 18 na 19 mahali watu waliifananisha na umeme pamoja na sauti ya tarumbeta.

"Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya barangumu, na ule mlima ukatoa moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali. Wakamwambia Musa, sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asije akasema nasi tusije tukafa."

Basi kwa nini Mungu hawezi akasema nasi waziwazi? Ni kwa sababu tutaogopa, ndivyo ilivyo asili ya dhambi yetu. Wakati mwingine ni katika ubatizo wa Yesu katika Yohana 12 msitari wa 20 hadi 29 inayosema kama ifuatavyo: Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha katika miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu: Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba wakisema, Bwana tunataka kumwona Yesu. Filipo akamwendea akamwambia Andrea; Kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu.

Naye Yesu akajibu akasema, saa imefika atukuzwe mwana wa Adamu. Amini amini nawaambia, chembe ya ngano isipoanguka nchi, ikafa hukaa hali iyo hiyo peke yake, bali ikifa hutoa mazao mengi. Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.

Mtu akinitumikia, na anifuate, nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo.Tena mtu akinitumikia Baba atamheshimu. Sasa roho yangu inafadhaika; nami nisemeje? Baba uniokoe katika saa hii lakini kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii. Baba ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza nami nitalitukuza tena. Basi mkutano uliosimama karibu walisikia, wakasema ya kwamba kumekuwa na ngurumo; wengine walisema, malaiaka amesema naye.

Wakati mwingine ilikuwa katika sura ya kwanza ya kitabu cha Ufunuo, mahali huyo Mtume Yohana anajaribu kuonyesha alichoona na kusikia. Ufunuo sura ya 1 msitari wa 10 hadi 15 pamoja inasema: "Nalikuwa katika roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu, ikisema haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Sirmna, na Pergamo, na Thiatira,na Sardi, na Filadefia,na Laodikia.

Nikageuka niiyone ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka nikaona vinara vya taa saba vya dhahabu, na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa mwanadamu, amevaa vazi linalofika matitini. Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama miali ya moto; na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imeshafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi"

Tukiachana na mifano hii yote labda mzuri sana ni ule umepeanwa na Eliya, wakati alikuwa amatorokea jangwani kutoka kwa walioitwa manabii wa Baali. Katika 1 Wafalme sura ya 19 msitari wa 9 hadi 16 pamoja, Eliya anaelaza hadithi yake ya kusikia sauti ya Bwana. "Akafika kunako pango, akalala ndani yake.Natazama neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, unafanyanini hapa, Eliya?

Akasema nimeona, wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako na kuzivunja madhabahu zako, na kuwauwa manabii wako kwa upanga; nami nimesalia peke yangu; nao wanifuata roho yangu, waniondoe. Mungu akasema toka usimame, mlimani mbele ya Bwana. Na tazama Bwana akapita; upepo mwingi wa nguvu ukipasua milima, ukaivunja vunja miamba mbele za Bwana lakini Bwana hakuwako katika lile tetemeko la nchi; na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini Bwana hakuwako kwa moto ule; na baada ya moto sauti ndogo ya utulivu.

Eliya aliposikia, alijifunika uso wake kwa mavazi yake, akatoka akasimama mlangoni mwa pango. Natazama sauti ikaja kusema, unafanya nini hapa Eliya? Akasema nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako na kuzivunja madhabahu zako, na kuwauwa manabii wako kwa upanga; name nimesalia mimi peke yangu; nao wananitafuta roho yangu waniondoe.

Bwana akamwambia, Enenda urudi njia ya jangwa la Dameski; ukifika, mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu; na Yehu mwana wa Nimshi mtie mafuta awe mfalme wa Israeli; na Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola umtie mafuta awe nabii mahali pako."

Kwa kuelezea sauti ya Bwana itafanana na sauti gani kwako, hakuna msitari mzuri zaidi. Kwa sababu Roho Mtakatifu anaishi ndani yako (iwapo wewe ni mkristo wa matendo sio wa maneno) na atazungumza na wewe kwa njia ambayo utaweza kutambua, lakini unaweza sikia na kufahamu kupitia misikio ya kiroho pekee.

Katika kilindi na kwa undani zaidi uhusiano wetu ulivyo na muumba wetu, ndivyo tunavyopata kuelewa hiyo sauti ndogo inaponena nawe. Moja ya njia ya haraka ya kukua kwa uwezo wako wa kufahamu hiyo sauti ndogo ni kuitii mara moja na ufanye chochote ambacho Mungu anakueleza ufanye. Hakuna uhusiano unaoweza kukua wakati mtu anaendelea kufanya vitu ambavyo vina chukiza mwingine.

Njia nyingine muhimu ni kukaa muda wakutosha na Mungu wakati wa asubuhi unapoamka toka kitandani. Hili ndilo Yesu alifanya na ilimshababisha yeye kukua katika uhusiano wake na Baba. Asubuhi mapema ndilo saa zuri ya kuwa na wakati wa kutosha kusikiliza ni nini Mungu anataka aseme nawe, kumwabudu na kusoma neno lake kabla na vikwazo vya siku kwa nguvu.

Mungu anataka kuwa na uhusiano wa wawili, kama vile mfalme Daudi alivyofanya katika Zaburi 142 msitari wa 1 na 2 unasema, "Kwa sauti yangu nalimwita Bwana, kwa sauti yangu nitamwomba Bwana dua. Nitafunua malalamiko yangu, shida yangu nitaitangaza mbele zake." Hivyo sivyo wafanyavyo watu walio katika uhusiano? Una shiriki na Mungu kitu kilio moyoni mwako naye ashiriki nawe kitu kilio katika moyo wake.

Uhusiano wowote uchukua muda kukomaa, na una panda shuka zake, hata hivyo Bwana anastahili kutafutwa kama "Vile ayara aoneavyo shauku maji baridi anywe katika kiangazi" kama vile kiitikio kinachojulikana sana kinasema. Uhusiano unastahili kujengwa katika hali ya kutokata tama, wakati wote endelea kutafuta na ukumbuke ahadi ya Mungu katika Yeremia sura ya 29 msitari wa 13 inayosema ifuatavyo: "Utakavyo nitafuta utanipata, utakavyo nitafuta kwa moyo wako wote."

back to main articles page