Fundisho la bibilia kuhusu Roho Mtakatifu.

Bible study on The Holy Spirit

Roho Mtakatifu ni nani?

Roha Mtakatifu ni sehemu kumbwa ya Mungu kama Yesu na Baba. Utaona kupitia maandiko yanayoonyesha Mungu kama utatu. Maelezo ya kwanza kwa Roho Mtakatifu yanapatikana katika mwanzo wa kitabu cha Mwanzo sura ya 1 ms 2 inasema hivi: "Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia katika uso wa maji."

Kabla hatuja angalia sehemu zingine katika agano la kale ninataka kwenda katika injili ya Yohana katika sura ya 14, mahali ambapo tunasoma zaidi kuhusu Roho Mtakatifu. Yesu anaongea na wanafunzi wake nini kichoenda kufanyika kwake karibuni, lakini hataki wasikie kana kwamba wataachwa kama yatima. Msitari wa 16 wa sura hii unapeana mfano wa kazi moja ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu.

"Nami nitamwomba Baba, naye atawapa msaidizi mwingine, iliakae nanyi hata milele". Kwa wazi basi tumepewa Roho Mtakatifu ilitupate kutiwa moyo wakati tunapitia nyakati mbaya na kuvunjika moyo. Sababu nyingine ya mwanadamu kupewa Roho Mtakatifu imeonyeshwa katika msitari wa 26 katika sura hiyo hiyo.

"Lakini huyo msaidizi huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote niliyowaambia" Tambua kwamba katika mistari hii Roho Mtakatifu anaonyeshwa kama mwanadamu. Jina "huyo" katika lugha ya Kingereza linaweza kutumika tu wakati unazungumzia kuhusu mtu.

Msitari unaendelea "Atawafundisha ninyi" -kuonyesha mtu tena. Fahamu hivi kuwa hii imanishi mtu kama mwanadamu lakini mtu wa ulimwengu wa Rohoni. Malaika pia ni watu. Hapa tunaona tena kusudi la kupewa Roho Mtakatifu na Mungu, ili aweze kuwa mwalimu wetu, na atukumbushe yote Yesu aliyosema na kutabiri.

Zaidi, kwa sababu Roho Mtakatifu ni sehemu ya Mungu atatuongoza katika kweli yote. Basi chochote mtu yeyote anasema, haijalishi sifa zake na elimu yake, haijarishi inasikika vyema, ichunguze na mwalimu wako, mwulize Roho Mtakatifu akuonyeshe ukweli au chochote kwa yaliyoandikwa au kusemwa.

Kwa ajabu, katika kutufundisha kweli, tunaposoma maandiko, Roho Mtakatifu wakati mwingine anatuleta katika ufahamu wa sehemu nyingine tunazo soma, ambazo hutukuwahi kuelewa wala kusikia awali, basi unamjua Roho Mtakatifu kama mwalimu wako. Msitari wa 17 wasura hii unaonyesha Yesu akifinua kitu kwa wanafunzi wake ambacho hawakuwa na wanafahamu kwa wakati huo.

"Kwakuwa anakaa ndani yenu na ataonekana kwenu" Baadaye tutaangalia msitari huu kwa undani, lakini kwa sasa hebu tuendelee kuangalia sehemu ya Roho Mtakatifu ambayo tunastahili kujua kuhusu. Mathayo 3 ms 16 inamwonyesha Yesu Kristo katika wakati wa ubatizo na Yohana mpatizaji katika mto Yordani. "Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama mbingu zika mfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake". Katika kufahamu hua, kando na kuwa myama mpole, pia ni makini sana na hawezi kutua mahali popote ambapo hayuko salama na hana furaha. Basi iwapotutaenda pamoja na Roho Mtakatifu katika maisha yetu ya kila siku lazima tuweze kumakinika, na kutoa chochote kinacho weza kumkashiliza.

Lazima tutafute kutoa chochote kilicho kibaya maishani mwetu. Hebu sasa tuende mbele tena katika Matendo ya Mitume mahali ambapo tutaweza kuona ni kwanini alama hii ya mwisho ni muhimu sana. Sura ya 1 mstari wa 8 unasema hivi, kunukuu Yesu kwa wanafunzi wake, "Mtapokea nguvu wakati Roho Mtakatifu atawajilia juu yenu".

Nguvu za nini? Kushuhudia kwa uwezo, na kuonyesha alimwengu ishara na miujiza ambazo zitaonyesha ulimwengu kuwa Yesu ndiye yule kweli unayemtangaza kuwa. Nguvu ambazo ziko hapa kwa ajili yako ni, zaidi ya nguvu zozote za adui ambazo zimetumika kinyume nawe mwenyewe kwa wakati mmoja, na zaidi ya hii baadaye.

Yesu yuko hapa anazungumzia majuma machache yalio mbele, na siku ijayo ya Pentekoste, wakati wanafunzi na wote katika chumba cha juu wanapokea Roho Mtakatifu kwa njia tofauti kuliko vile waliwahi hapo nyuma, iwapo utatazama nyuma katika injli ya Yohana Mtakatifu, sura ya 20 msitari wa 22 una nakili Yesu akiwavuvia wanafunzi wake akisema pokeeni Roho Mtakatifu.

Yesu anaingia ndani ya kila muumini, wakati ule amempokea Yesu Kristo katika maisha yao kama Bwana, Mwokozi, na Mungu. Kwa wazi kilichofuatia siku hii ya Pentekoste kilikuwa tofauti tena. Ni somo ambalo tutaliangalia wakati ujao.

(2) Roho Mtakatifu katika agano la kale lote.

The Holy Spirit Throughout The old Testement

Ifuatayo ni mtazamo mfupi wa maelezo ya wazi kuhusu Roho Mtakatifu na kazi ya Roho Mtakatifu katika Agano la kale. Umeona kutoka Mwanzo sura ya kwanza kuwa Roho Mtakatifu kuwako katika nyakati za kwanza za uumbaji, kama vile kuna maelezo mengi tutaangalia tu machache Hesabu 11 ms 17-Hapa Musa amemlalamikia Mungu kuwa, mzigo wa kujaribu kuongoza, kutiamoyo na kuchunga watu zaidi ya nusu milioni ni mzito sana kwake. Mungu basi anakubali kuwa atapeana sehemu ya upako ulio juu ya Musa kwa sehemu ya wengine, ilikusaidia Musa kwa kazi yake.

Hesabu 11 ms 26 nionyesho lingine kuhusu kilichofanyika katika siku za Agano la kale wakati Roho Mtakatifu alimjilia mtu. Hii inafanyika wakati mwingine siku za leo. Hesabu 11 ms 29-Ana dhihirisha nia ambayo kwa hakika ilikujatimia miaka 3000 babadaye. Waamuzi 6 ms 34-ni mfano wa mtumishi wa Mungu akiwa ametiwa nguvu kwa ajili ya huduma ambayo hata hivyo hangeweza kufanya ni kuwezeshwa kwa kiungu.

Waamuzi 13 ms 25 inaonyesha kuinuka kwa mtu wa Mungu, katika huduma, hili ndilo tunastahili kutia moyo katikati yetu. 1 Samueli 16 ms 13 – inaonyesha vile roho Mtakatifu anamtia mafuta mtu kwa ajili ya kazi ya huduma, kumwezesha na kumtia nguvu. Baada ya hii Daudi ailishiriki mambo magumu mengi lakini akapenya na akaona kufaulu ambako Mungu alimletea. Ezekieli 3 ms 4 –Hapa nabii Ezekieli anaelezea kuhusu Roho Mtakatifu akija juu yake na nini kilichofanyika kama matokeo yake.

Watu kupokea maono na mambo fulani muhimu kutoka kwa Mungu kwa pamoja kwa njia ya ajabu ni jambo finyu sana kama vile wengine wanafikiria hilo kuwa. Inafanyika kila wakati. Ezekieli 36 ms 27 – hii ni ahadi ya Mungu nitakayokuwa nina iangazia nyuma baadaye katika somo hili. Musa alikuwa amedhihilisha nia yake kuwa kila mtu angeweza kutabiri – hii ni ahadi nyingine kutoka kwa Mungu kuwa siku ambayo Musa aliitamani kufika kwa hakika itatimia.

Yoeli 2 ms 8 – wengi wana amini kwamba ahadi hii haijatimizwa kabisa. Nina amini tunaenda hivi karibuni kushuhudia utembezi wa Mungu katikati ya Wahindi, Waislamu, Makarasinga na watu wengine wameletwa pamoja sio kupitia wamishonari, lakini kupitia maombi na matendo ya ukuu wa Mungu.

Kwa wakati mwingi sasa nina sikia kuhusu makundi ya Kiislamu, ambao viongozi wao wamepewa ufunuo wa ndani wa Yesu ni nani, na wameleta kundi lao kujua Yesu Kristo, na kumpokea katika maisha yao kama mwokozi, Masihi na Bwana nina animi hii inaenda kufanyika kwa upana zaidi na kwa wakati mwingi katika siku hizi za mwisho.

Mwisho mstari muhimu unaoonyesha jinzi mambo yote yatakavyofanywa, Zakaria 4 ms 6 unasema "Sio kwa nguvu wala sio kwa uwezo, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi" Kama vile watu wa Mungu katika siku za Agano lake wahitaji kupewa nguvu na Roho Mtakatifu, ndivyo nasi katika siku hizi za mwisho. Jinsi ya kupokea nita waonyesha katika fundisho letu la mwisho.

3) Roho Mtakatifu katika Agano Jipya

The Holy spirit in The new Testement

Hata hivyo njia tano tofauti za kwelezea kazi ya Roho Mtakatifu zinapatikana katika Agano Jipya.

Mfariji (Yohana 14ms16)

Comforter

Yesu akiwa tayari kuondolewa kutoka ulimwengu huu na usoni mwa wanafunzi wake, njia nyingine itahitajika kwa ajili ya watu wa Mungu kujua kweli ya Mungu, bila hivyo watakuwa na hasara bila Yesu (kama inavyooyeshwa wao wamejitenga na kujifungia mbali katika chumba cha juu kwa hofu ya Wayahudi kabla yesu hajawatokea baada ya ufufuo wake) Walidhania mambo yamefika mwisho, walikuwa wadhaifu, wamevujika moyo na wakiomboleza. Wakati Roho Mtakatifu aliwajilia na kuanza kukaa ndani yao katika Pentekoste walikuwa wamebadilishwa. Wenye nguvu katika imani na ujasiri (kujiamini) kwa Mungu, wenye uwezo (nguvu halisi za kutosha) na wenye kumwelewa Mungu katika maisha yao kupitia uhusiano wao wa ndani na yeye.

Roho wa Kweli (Yohana)

The Spirit of truth

Ni Roho Mtakatifu atakaye tuongoza katika kwaeli yote mbali na uongo. Anafanya hivi kwa kutupatia utambuzi ilikwamba tuweze kuangalia kile tumesikia tuonekama nicha kweli au la. Kwa Mungu hakuna chochote cha uongo, Hatajaribu kutusukuma sisi tufuate chochote ambacho sio kweli kamili. Mungu habadiliki, Viwango vyake havibadiliki na neno lake halibadiliki pia.

Hata wakati tunasikia tuko mbali na Mungu tunaweza jua kweli kuwa yuko pamoja nasi wakati wote. Wakati tunaona kuwa tumeonewa tunaweza jua kweli kuwa ata weza kulipiza zaidi ya haki ambayo tumedhurumiwa. Wakati tumekaliwa na kujihukumu tunaweza jua kweli, kuwa Mungu hawezi akatupenda upendo mdogo kuliko wakati tumefanya kwa bidii yetu. Iwapotuta kiri dhambi zetu, yeye ni mwaminifu wa kutusamehe sisi na kututakasa na uovu wote. (Sio juma lijalo, sio mwezi ujao, lakini hivi punde.

Mwalimu Yohana (14ms26)

The teacher

Wakati tunakuwa na uhusiano na Mungu kupitia Yesu, Roho Mtakatifu mwenyewe atatufundisha mambo ya ajabu. Wakati mwingine tunapojitenga na yeye kwa ajili ya maombi, au kusoma bibilia binafsi, Roho Mtakatifu atatufundisha mambo, wewe tu na Yeye. Wakati mwingine kupitia mahubiri na mafundisho ya bibilia katika mkutano Roho Mtakatifu atakufanya hapo kwa hapo ukumbuke neno andiko katika bibilia labda hata ufupi wa yalio semwa. Nina sema tena, chochote kinachonenwa na yeyote anaye nena, kiangalie na Mungu iwapo ni kweli.

Mfunuaji (Yohana 16ms13)

The revealer

Wakati mwingine unaposoma bibilia peke yako pamoja na Mungu, na katika maombi, Mungu ataanza kukuonyesha jinzi anavyohisi kuhusu hali fulani, au akuonyeshe jambo ambalo ataenda kulifanya katika siku zijazo. Iwapo hii itafanyika kwako ichunguze na mtu wa kuaminika. Mungu wakati mwingi atawafunulia wengine mambo yanayofanana.

Labda unapokuwa ukisema, mtu anayekuwa anazikiliza ataitambua kama ufunuo wa kweli kutoka kwa Mungu, au labda Mungu ame waonyesha kitu hicho hicho, Kwa mfano Mwingereza mmoja alidhani alikuwa akiambiwa aende mpaka sehemu Fulani katika mduara wa artic na aombe kwa ajili ya kuwa achiliwa kwa wafungwa na waliokandamizwa katika nchi za magharibi.

Akihisi kuwa hili ni jambo la ajabu kufanya (kwa nini asifanye aikwa nyumbani?) hata hivyo akatoka akatii. Akaomba kwa muda wa masaa 8 hivi na kisha kuhisi ni mpubavu, akarudi tena hoterini kwa njia nyingine. Akiwa maili nusu amwona mzee amesismama peke yake, akiwa ameipatia kusini kisogo ameangalia katika sehemu ya kazkazini-mashariki.

Kile ambacho yeyote kati yao hakujua nikuwa kila nusu maili kwa zaidi ya maili hamsini kumesimama mtu aliye peke yake, akiwa anajiona mpumbavu lakini ana mzigo wa kuomba. Huna yeyote kati yao alijua kuwa wamefanya sehemu ya maombi ya mnyororo. Baada ya miezi michache na serikali ya kikomunisti ikaanza Poland. Ujerumani (mashariki) na Urusi.

Mungu alikuwa amefunua moyo wake kwa waliokandamizwa katika mataifa ya mashariki, na akawatuma waende kuomba ili watu wake waweze kuwa na nafasi ya kuchagua kuwa huru. Wakati mwingine baada ya miaka ukiwa unashangaa andiko Fulani lilikuwa lina maanisha nini kwako, utakuja kulifahamu kwa ghafla kwa kuwa limefunuliwa kwako. Vipawa vya ufunuo ni pamoja na: unabii, neno la maarifa na hekima.

Mwezesha (Matendo 1ms8)

Empowerer

Katika Pentekoste wanafunzi waliwezeshwa kufanya kazi za ajabu, na miujiza kwa sababu walifuata mafundisho, na uvuvio wa Roho Mtakatifu ,kama alivyo wawezesha kufanya miujiza ambayo Yesu alikuwa akifanya katika maisha yake duniani. Maelifu ya makanisa yanaanza kutambua tena miujiza ya uponyaji, na idadi kumbwa ya wanaokoka kama vile wanavyo mruhusu Roho Mtakatifu afanye kazi yake katika kanisa zao na mikutanoni.

Usiogope kile kinachoweza kutokea, kwakuwa Mungu ni mpole, mkarimu na mwema. Omba na atakupa utambuzi kwa vitu vile ambavyo ni vya Mungu na vile visivyokuwa, na hekima ya kujua tofauti na jinsi unavyoweza kukabiliana na mambo ya sio kuwa ya Mungu. Je, uko tayari kusimama kutoka kwa chokaa-mwanga na uruhusu Roho Mtakatifu aongoze mikutano yako? Atakuja iwapoutamwita kwa moyo wako wote!

Ni nini ubatizo wa Roho Mtakatifu?

What is the baptism of the Holy Spirit

Katika Ezekieli 36 ms27 Mungu ana ahidi kuwa siku inakuja atakayotia Roho yake ndani ya watu wake. Yoeli nabii akasema wakati utakuja ambao Mumgu atamwaga Roho wake Mtakatifu juu ya wote wenye mwili. Tumeona kupitia mafundisho ya Roha Mtakatifu katika Agano la kale tofauti inayaweza kufanya wakati Roho Mtakatifu amemjilia mtu.

Katika matendo 1 ms 8 Yesu anawaahidi wanafunzi wake "mtapokea nguvu wakati Roho Mtakatifu atakapo wajilia) Nguvu za kufanya? Kuonyesha kwa ishara na maajabu ya kuwa Yesu ni yote kama vile Maandiko yanamwonyesha kuwa, na nguvu za kushuhudia wengi na kuhubiri na nguvu nyingi na ufanisi wakati tunatangaza kweli za bibilia kwa ulimwengu.

Hata leo, nguvu hizo hizo za kushuhudia na ishara na miujiza zinapatikana kwa ajili yetu kwa uhuru iwapo tutajifungua wenyewe kwake. Jina ubatizo lina maanisha kutumbukiza, kuloweka kabisa (mtu au kitu) kutoka nje (inawezekana pia kwa ndani). Yohana mpatizaji amenakiliwa katika injili ya Yohana Mtakatifu sura ya 1 ms 34 akiwa ameleza Yesu kama mmoja ambaye atakubatiza wewe kwa Roho Mtakatifu.

Mara unapopokea ubatizo huu na nguvu, utahitajika kujifundisha kuitumia kwa njia ambayo Mungu alikusudia itumiwe. Katika Efeso 5 ms 18 Paulo anatusihi sisi tujazwe na Roho Mtakatifu. Nimeambiwa ya kuaminika kuwa kutoka tafsiri ya awali ya kuwa himizo hili liliandikwa katika hali ile ya kuendelea.

back to main articles page